Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Na Blogs za Mikoa Tanzania.
kuna haya maneno yanasema kuwa Ardhi ni moyo wa mwanamke katika kujikomboa kimaisha
kuna haya maneno yanasema kuwa Ardhi ni moyo wa mwanamke katika kujikomboa kimaisha
Pamoja
na jitihada mbalimbali za kumwendeleza mwanamke katika kujikwamua na umaskini
raslimali ya ardhi ndiyo chachu kubwa ya kuwawezesha wanawake kujikwamua na
umaskini hapa nchini.
Mwanamke
mwenye umri wa miaka 54 anaetambulika kwa jina la Zaharia Ally mkazi wa Bumbuli
wilayani Lushoto, mkoani Tanga ni miongoni mwa wanawake wanye changamoto za
maisha na wanaopambana kujenga familia zao.
Mwanamke
huyo ambaye ni mjane na mlemavu wa mguu amekuwa akijikita katika kilimo jambo
linalomuwezesha kuweza kujikimu kimaisha na familia yake yenye watoto wanne.
Ingawa
mwanamke huyo ni mjane kwa zaidi ya miaka 15 kilimo kimekuwa mkombozi mkubwa
kwake baada ya na kuonyesha ukomavu kwamba mwanamke akitambua wajibu wake
katika familia hata akipatwa na matatizo anapambana kuhakikisha anamudu
majukumu yake kama mama katika familia.
Kwa
mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania wananchi
wanaojihusisha na kilimo na ufugaji ni zaidi ya asilimia 70% ambapo wanawake
ndiyo chachu ya maendeleo katika kazi zote hizo.
Wanawake
wanaadhimisha siku yao tarehe 08.03 2016 ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu
inasema '50 kwa 50 ifikapo 2030 tuongeze jitihada'.
Siku
hii huwa ni mahsusi kwa wanawake kukutana katika maeneo mbalimbali na
kukumbushana mambo muhimu katika kuondokana na mfumo dume katika jamii na
kupiga hatua za maendeleo.
Hata
hivyo taasisi binafsi pia zitajumuika katika siku hiyo ambapo Oxfam Tanzania kupitia
mradi wake wa Grow unaoendesha shindano la mama shujaa Wa chakula watakua mkoani Mtwara kushererekea na
kutoa ujumbe kwa jamii hasa umiliki Wa ardhi kwa wanawake
No comments:
Post a Comment