HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » LEO KATIKA HISTORIA: MUAMMAR GADDAFI KIONGOZI ALIYEINGIA MADARAKANI KWA MAPINDUZI YASIYO YA KUMWAGA DAMU

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Muammar Gaddafi alikuwa ni tofauti na viongozi wengine waliowahi kutajwa kuwa madikteta duniani, ana mengi ya kukumbukwa na kusifiwa kwayo. Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuongozi wamekuwa wakieleza kusikitishwa kwao na kutotambua aina ya demokrasia ambayo baadhi ya watu wa Libya wanaililia kwa sasa na iwapo itaboresha au kuharibu kabisa maisha yao.
Muammar Gaddafi alizaliwa Juni 7, 1942 katika mji wa Sirte, katika familia ya Mohamed Abdulsalama Abuminiar na mama Aisha Ben Niran. Alijiunga na Jeshi la Libya mwaka 1965.
Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri na Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.
Gaddafi alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi na aliwahi kupata mafunzo zaidi akiwa Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya katika mji wa Benghazi, na kupanga mapinduzi ya tarehe 1 Septemba mwaka wa 1969.
Aliongoza Libya tangu alipompindua Mfalme Idris I, katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu, wakati huo akiwa na umri wa miaka 27.
Gaddafi alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.
Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa iliyojumuisha kanuni za kiislamu na mfumo uliyo tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.
Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.
Gaddafi aliitawala Libya kwa miaka 42 tangu mwaka 1969, pia aliwahi kunadi wazo lake la kuungunisha nchi za Kiarabu, ambalo lilishindikana.
Gaddafi alikuwa maarufu kwa nguo alizopenda kuvaa, na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa, kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.
Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am na hapo Umoja wa Mataifa ukaondoa vikwazo dhidi ya Libya.
Baada ya miezi kadhaa, serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za magharibi.


Hapo ndipo mabadiliko halisi yalionekana kwa kuwa nchi hizo za magharibi zilibadili mtazamo wao na kuacha kumtenga Gaddafi na kushirikiana naye hata kama alikuwa hatabiriki.
Mfumo huo wa Gaddafi ulivuka mipaka na haukuhusisha mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.
Akiwa safarini ng'ambo, alikuwa anakaa kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.
Hema hiyo pia lilitumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.

Muammar Gaddafi na Tony Blair waliwahi kuandaa mkutano wa viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 29 Mei 2007 kwenye hema hiyo ya Kibedui.

Kanali Gaddafi alijitahidi kwa muda mrefu kutoa ushawishi wake nyumbani na ng'ambo.
Awali alituma jeshi lake nchini Chad ambapo wanajeshi walidhibiti ukanda wa Aozou, kaskazini mwa nchi hiyo, mwaka 1973.
Katika miaka ya 80 aliandaa mafunzo kwa makundi ya waasi kutoka Afrika Magharibi yaliyojumuisha wale wa Tuareg ambao ni Waberber.

Jumuiya ya wanadiplomasia waliitenga Libya kutokana na Kanali Muammar Gaddafi kuunga mkono makundi yeneye silaha, ikiwemo Irish Republican Army na Palestine Liberation Organisation.
Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.
Ilisemekana kuwa Kanali Gaddafi alitikishwa na mashambulio ya mabomu hayo ambapo mtoto wake wa kike wa kufikia aliuawa.
Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.
Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.
Wakati wa mabadiliko katika karne ya 20, huku Libya ikiwa inapata tabu kutokana na vikwazo dhidi ya nchi hiyo, alianza kurekebisha hali nchini mwake.
Mwaka wa 2003, mabadiliko yakaanza kuonekana na baada ya miaka mitano mkataba wa kulipa fidia kwa waathirika wa Lockerbire uliafikiwa na hii ikarejesha uhusiano kati ya Washington na Libya.
'Hakutakuwa na vita tena, mashambulio, na vitendo vya ugaidi' Kanali Gaddafi alisema alipokuwa akiiherehekea miaka 39 aliyokaa madarakani.

Kiongozi huyo wa Libya hujiona kama kiongozi wa kidini wa taifa hilo, akihakikisha kwa kile anachosema ni demokrasia.

Wanaompinga aliwakandamiza kikatili na vyombo vya habari vilibaki katika udhibiti mkubwa wa serikali.
Libya ilikuwa na sheria ambazo haziwaruhusi watu kukusanyika katika misingi ya kisiasa zinazopinga mapinduzi ya Kanali Gaddafi.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilisema serikali hiyo imewatia mbaroni mamia ya raia kwa kukiuka sheria hiyo na baadhi yao kuhukumiwa kifo.
Inadhaniwa kuwa Kanali Gaddafi aliandaa namna ya kukabidhi madaraka yake kwa sababu ya umri aliyofikia lakini haijulikani ni nani atakayerithi uongozi wa Libya kutoka kwa Gaddafi.
Ilisemekana kuwa mwanawe Sayf Al-Islam Gaddafi ndiye atarithi uongozi kutoka kwa baba yake na ataongoza katika kuleta mabadiliko.
Wanandoa wote wapya nchini humo walipata Dola 50,000 kwa Serikali kwa ajili ya kununua makazi yao kuwasaidia kuanzisha familia mpya.Elimu na huduma za kiafya vilitolewa bure. Wakati Gaddafi nachukua nchi asilimia ya waliokuwa na elimu ilikuwa 25, kwa sasa inafikia 83.
Gaddafi aliwahi kusisitiza kwamba wazazi wake hawawezi kupata makazi hadi kila raia apate makazi. Baba wa Gaddafi alifariki dunia wakati yeye, mama yake wakiwa wanaishi katika hema.
Hakukuwa na riba katika mikopo, benki zote Libya zilikuwa chini ya Serikali, mikopo ilitolewa kwa wananchi bila riba ya kiasi chochote .
Gaddafi aliapa kuipigania nchi yake hadi tone lake la mwisho la damu. Alitimiza kiapo chake hicho kwani alifia ndani ya ardhi ya mababu zake na damu yake ilimwagika ndani ya ardhi ya babu na bibi zake katika shambulizi la mwisho kabisa la kuuteka mji wake wa asili wa Sirte ambao alilazimika kukimbilia baada ya mji mkuu wa Tripoli na makazi yake kutekwa Agosti, mwaka 2011.
Kanali Gaddafi aliuawa Oktoba 19, mwaka 2011 baada ya mapambano ya takriban miezi saba na waasi wa nchi hiyo ambao walikuwa wakiungwa mkono na mataifa ya Jumuiya ya Kujihami ya Ulaya Magharibi (Nato), tangu Februari mwaka 2011 baada ya machafuko katika nchi za Tunisia na kisha Misri. na majeshi ya waasi waliojipachika jina la Baraza la Mpito (NTC).

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: