Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya vyama vinne vyenye uwakilishi bungeni vitarejea bunge lijalo kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili sintofahamu kwa vyama hivyo katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa vyama vya upinzani nchini vimemshauri Rais John Pombe Magufuli kuvifuta vyama vya upinzani kama anaona vinamsumbua anapofanya mambo yake.
Hayo yamesemwa leo na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia ambapo amesema kuwa kama Rais Magufuli anaona vyama vya upinzania vinamkera na kumkwamisha anapotaka kufanya jambo basi serikali yake ipelekea mswada kwa hati ya dharura bungeni ili kufanya mabadiliko katika sheria ya vyama vya siasa na kuvifuta vyote.
Mbatia amesema kuwa jambo hilo amelitafakari na kuwashirikisha viongozi wenzake na huenda ikasaidia kwa sababu Rais Magufuli anaonekana kutaka kuongoza kwa kutumia akili yake na hataki kukosolewa na mtu yeyote wala chama chochote.
Katika hatua nyingine, viongozi wa vyama vya upinzani wameitikia wito wa viongozi wa dini uliowataka kurudi bungeni na wameahidi kuwa watajadiliana na wanaamini watafikia muafaka na kurudi bungeni katika mkutano ujao mwezi wa tisa.
No comments:
Post a Comment