Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
(katikati) akiongea wakati wa ufunguzi
wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika inayoratibiwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa wadau wa utamaduni
leo Jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Mtaalam wa Utamaduni wa UNESCO Bi. Rehema Sudi
anayefuatia ni Mtaalam wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya na wakwanza
kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bibi. Deirdre Solani
Mtaalam
wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya (katikati) akizungumza wakati wa
ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika kwa wadau wa
utamaduni iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni(UNESCO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni
Mtaalam wa Utamaduni wa UNESCO Bi.
Rehema Sudi.
Mtaalam
wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya (katikati) akizungumza wakati wa
ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika kwa wadau wa
utamaduni iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni(UNESCO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni
Mtaalam wa Utamaduni wa UNESCO Bi.
Rehema Sudi.
Na: Genofeva Matemu
Serikali imeahidi kuhifadhi kumbukumbu na takwimu sahihi za urithi wa
Utamaduni usioshikika kwa lengo la kuuendeleza na kuiwezesha jamii kuulinda kwa
ajili ya vizazi vijavyo.
Rai hiyo imetolewa na
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabriel alipokua akifungua warsha ya siku kumi iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa
warsha hiyo Prof. Gabriel amewataka washiriki kujifunza vizuri ili baadaye
waweze kusaidia katika kuwekeza, kuibua,
kutambua na kutunza urithi wa utamaduni ushioshikika kwani hiyo ndio njia mojawapo
itakayowavutia watalii wengi kuja nchini
kujifunza tamaduni zetu zisizoshikika.
“Utamaduni ni nta
inayowaweka watu pamoja, ni vyema mafunzo haya na utaalamu mtakayoipata izingatie
kuibua fursa na kutambua tamaduni ambazo hazishikiki kwani serikali ina malengo
na matumaini makubwa sana kutoka kwenu” alisema Prof. Gabriel.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Msaidizi Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Bibi. Lily Beleko amesema kuwa Tanzania iliweka saini na kuridhia
mkataba wa kulinda urithi wa utamaduni usioshikika ambao ulipitishwa na Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzaia mnamo mwaka 2011.
Anaongeza kuwa baadaye UNESCO kwa kushirikiana na Wizara inayohusika
na mambo ya Utamaduni wamekua wakishirikiana katika kutoa mafunzo kwa wadau wa utamaduni na watu
binafsi kuhusu namna ya kuhifadhi
urithi wa utamaduni usishikika ambapo mafunzo hayo yanafanyika kwa mara
ya nne sasa huku lengo likiwa ni kutekeleza mkataba huo.
Aidha Bibi. Beleko
amesema kuwa watanzania wengi wamekua wakidhani kuwa utamaduni ushioshikika
unahusiana na mambo ya kichawi hivyo
kutotilia maanani umuhimu wake kitu ambacho si kweli kabisa kwa kuwa maana
halisi ya utamaduni usioshikika unahusisha vitu vinavyohusiana na mazingira, maendeleo
ya watu pamoja na mila na desturi zao yakiwemo maongezi, nyimbo, maigizo,
midundo ndani ya ngoma ambayo yanaambatana na ala.
Naye Mwakilishi
kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bw.
Mathias Luhanya amesema kuwa dhumuni la warsha ni pamoja na kuwajengea uwezo
wadau wa utamaduni namna ya kuhifadhi urithi wa utamaduni usioshikika ili
baadaye waweze kuorodhesha urithi huo kwani Tanzania ina bahati ya kuwa na
jamii zaidi ya 120 hivyo ni matarajio kuwa urithi wa utamaduni usioshikika
umesheheni ndani ya kila jamii.
No comments:
Post a Comment