Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

MARA nyingi paka wa nyumbani huwinda usiku. Imegundulika kwamba sharubu huwasaidia kutambua vitu na kukamata windo hasa baada ya giza kuingia.
Sharubu za paka zimeunganishwa na tishu zenye mishipa mingi ya fahamu. Mishipa hiyo ina uwezo mkubwa wa kutambua hata msukumo mdogo wa hewa.
Hivyo, paka wana uwezo wa kutambua vitu vilivyo karibu nao bila kuviona, jambo linalowafaa kunapokuwa na giza.
Kwa kuwa sharubu zina uwezo wa kutambua shinikizo la hewa, paka huzitumia kujua mahali na mwendo wa windo au kitu fulani. Pia, sharubu husaidia paka kupima upana wa sehemu fulani kabla ya kuingia.
Kitabu Encyclopædia Britannica, kinasema kwamba “kazi ya sharubu (vibrissae) inajulikana kwa kiwango kidogo tu; hata hivyo, paka hulemaa kwa kipindi fulani cha wakati sharubu hizo zikinyolewa.”
Imeandaliwa na Moses Mutente.



No comments:
Post a Comment