HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » JESHI LA POLISI WAKAMATA SILAHA MBILI ZA KIVITA MKOANI RUKWA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Silaha mbili za kivita zimekamatwa Mkoani Rukwa majambazi walipokuwa wakijiandaa kufanyia uhalifu katika kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya ambapo watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo baada ya kukutwa na silaha hizo zisizoruhusiwa kumilikiwa na mtu yeyote hapa nchini.

Silaha hizo mbili aina ya SMG zenye namba ya usajili UC-1089-1998 na UC-763703 zimekamatwa baada ya raia wema kubaini wamiliki hao walipokuwa wakijiandaa kufanya uhalifu na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Kamanda Kyando amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wanaoutoa kwa polisi mkoani Rukwa na kuwahakikishia usalama wakati wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: