HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » » » » RIDHIWANI KIKWETE AFUNGUKA KUHUSU BIFU ZILIZOPO KWENYE MUZIKI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


Mbunge wa Jimbo la Chalinze na mtoto wa Rais mstaafu wa Tanzania wa awamu ya nne, Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunguka kuhusu bifu za wasanii zinazoendelea kwenye muziki hapa nchini.
Ridhiwani ameiambia Bongo5 wakati wa uzinduzi wa video mpya ya Belle 9 ‘Give It To Me’ Jumamosi hii uliofanyika kwenye beach yake maeneo ya Kawe jijini Dar kuwa wasanii wanatakiwa waache malumbano na waangalie kwenye kujiwezesha zaidi ili waweze kuwa juu kuliko walipokuwa jana.
“Mimi ningewaambia hawa vijana wetu ambao hasa wameanza malumbano kwenye muziki. Tumeshuhudia nchi ikimpoteza mwanamuziki mzuri kama Tupac na Notorious B.I.G kwa sababu ya mambo ya kijinga jinga na yasiyofaa kama haya, wajifunze katika hayo,” alisema Ridhiwani.
“Waache kuangalia nani anafanya nini, waangalie wao wanajiwezeshaje kuwa bora kuliko walivyokuwa jana, watafanikiwa,” ameongeza.

Chanzo: Bongo 5

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: