HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MFANYABIASHARA YUSUF MANJI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji (41) na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka saba ya uhujumu uchumi na usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh 200 milioni na mihuri.
Mbali na Manji wengine walioachiwa huru ni Deogratius Kisinda(28), Abdallah Sangey(46) na Thobias Fwere (43).
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo Alhamisi amewaachia huru washtakiwa hao saa saba mchana mara baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa kuomba ifutwe kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka hayo dhidi ya washtakiwa hao na Mahakama ikaridhia.
Akiwasilisha ombi hilo mahakamani hapo, Wakili Kishenyi amesema kuwa leo yaani siyo tarehe ya kesi hiyo, ila waliomba hati ya wito ya mshtakiwa (Remove order) na kuiarifu Mahakama kuwa DPP kwa niaba ya jamuhuri hakusudii kuendelea kuwashtaki washtakiwa hao katika kesi hiyo na akaomba iondolewe chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20.
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa washtakiwa hao, Hajra Mungula aliusema sheria hiyo inaruhusu DPP kuwaachia huru washtakiwa na pia inaruhusu kuwakamata.

Chanzo: Mwananchi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: