Najua kuwa hadi sasa ukifanya tafiti vijana wa umri wa miaka 20 hadi 30 ndio wanao ongoza kwa kusumbuka na matatizo haya ya nguvu za kiume tofauti na matarajio yetu wote kuwa tatizo hili tunasoma kuwa linawapata wazee, swali la kujiuliza kwa nini sasa vijana tena katika umri mdogo? Ndio maana nimeamua kukuandikia Makala hii ambapo kama ni miongoni mwa watu wanaosumbuka hili tatizo nina uhakika tatizo lako utapata suluhisho kutokana na elimu hii rafiki yangu. Pia najua unaweza ukawa na mchumba wako, unavumulia mengi kuhusu tatizo hili la mwenzi wako, usiwe mkimya kwani inahitaji utashi wa juu sana kumweleza mwenzi wako kuhusu hili swala kwani upungufu wa nguvu za kiume unasababisha msongo wa mawazo wengine hupelekea hadi kuchanganyikiwa hatimaye kupata MAJOR DEPRESSIVE DISORDER na mbali na hivyo husababisha kutokujiamini na woga wa kuwa na mke na hivyo wengi wamejaa wasiwasi na hofu kubwa ya kugunduliwa na mwezi wake kuwa ana tatizo hilo, na wengi wao ni woga sana kutogunduliwa tatizo hilo,ndio maana inapofikia hatua mwenza wako umembaini ni mara chache sana atakubali kuwa kweli ana tatizo hilo. Kwa nini usumbuke na matatizo kama haya wakati msaada wako upo? Usiendelee kusumbuka na tatizo hili kwani umeumbiwa maisha ya furaha na Mungu ni haki yako kufurahia uumbaji wa Mungu, anza leo kushughurikia tatizo kabla halijawa sugu mpendwa msomaji wa Makala hii.
NINI KISABABISHI MSINGI WA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME?
Katika mwili wa binadamu kuna vichocheo aina ya Testosterone
ambavyo hutolewa malengo ya kuimarisha utendaji kazi wa ubongo,ufanye kazi
katika hali tulivu,kuondoa,kuondoa msongo,kuondoa mstuko wa aina yoyote
,kuimarisha uwezo wa kufikiri,kuimarisha furaha ya mwili wako na hatimaye
kuimarisha nguvu za kiume na hatimaye kufurahia tendo la ndoa. Kazi kubwa ya
kichecheo hiki ni kuhakikisha mwili wako unakuwa katika hali tulivu kabisa kwa
kuutuliza ubongo wako ndipo utafurahia ndoa yako rafiki yangu.
Sasa endapo kichecheo hiki kikivurugika kinasababisha vichocheo
vingine kama insulin,leptin,cortisol,vichocheo vya ukuaji pia kuvurugika kwani
matokeo ya hitililafu hii mwilini inasababisha
KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME kwa sababu vichocheo hivi vinafanya kazi kwa
ushirikiano mkubwa, na endapo kimoja tu kikivurugika vyote vinapoteza mwelekeo
na tatizo kuwa sugu Zaidi.
Napenda leo nieleze kwa kina kidogo namna gani nguvu za
kiume zinapotea kutokana na mvurugiko wa vichocheo hivyo vikuu vitatu kama
nilivyo vitaja hapo juu.
1.
TESTOSTERONE
Kichocheo hiki ndio silaha ya mwanaume
kwani ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe na sifa zote za kiume na ndicho
kicheo ambacho kinakufanya uwe imara katika tendo la ndoa. Upungufu wa kicheo
hiki kinasababisha kupungua kwa matamanio kwa jinsia tofauti,kupungua kwa nguvu
za misuli yako kiutendaji,mafuta kurundikana ovyo mwilini( BELLY FAT AND
OBESITY)
Lakini pia ijulikane kuwa kichocheo hiki
cha testosterone sio kwamba kinapatikana kwa wanaume tu, la hasha! Kichocheo
hiki hata wanawake wanacho ingawaje kwa kiwango cha chini sana, endapo
kinapokuwa kimepungua kinaweza kumsababishia mwanamke kukosa matamanio kwa
jinsia ya kiume wakati wa tendo la ndoa, kukosa nguvu ya misuli ya kuhimili
tendo la ndoa (Kuchoka Sana),kuongezeka uzito kupita kiasi na nyama uzembe pia
kupunguza uwezo wako katika kufikiri na kumbu kumbu.
NINI KINASHUSHA TESTOSTERONE MWILINI MWAKO?
Moja ya kisababishi kikubwa cha testosterone
kushuka kiwango chake ni kwa sababu ya kuwepo na kizuizi cha insulin (insulin
resistance) hii inafanya kiwango cha insulin kuwa juu sana na kusababisha
testosterone kushuka kiwango chake. Moja ya sababu zinazo sababisha kiwango cha
insulini kuwa juu sana ni unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi kama soda na
pia ulaji wa vyakula vyenye vionjo mbalimbali vitamu vilivyotengenezwa
viwandani. Hivyo basi sukari inapokuwa ipo katika kiwango cha juu sana kwenye
damu inasababisha utolewaji wa insulin kuwa katika kiwango cha juu pia kwenda
kusawazisha sukari irudi kawaida. Hivyo basi matumizi ya vyakula na vinywaji
vya sukari nyingi vinafanya mwili upate kizuizi katika utendaji kazi wa insulin
na hatimaye testosterone pia kushuka kiwango chake. Najua umejifunza sasa kwa
nini watu wanaotumia vyakula vya viwandani,vinywaji vya sukari nyingi,ulaji wa
vyakula vyenye mafuta mabaya jinsi gani inasababisha vichocheo vyako kushuka
kiwango na unaendelea kusumbuka sana. Napenda kukuambiwa kuwa siku zote watu
hawaogopi vyakula vyenye sukari wanaogopa vyakula vyenye mafuta mengi, hio ni
fikra potofu sana! Sugar is more addictive than heroin and cocaine, kwa maana
nyingine watu ni walevi wa vyakula na vinywaji vya sukari na haipo siku anaweza
kuacha haraka. Usihofu kama una tatizo hilo ujue tayari umeshaathiriwa na ulaji
wa vyakula na vinywaji hivyo.
2.
INSULINI
Hiki ni kichecheo ambacho hutolewa na
kongosho lako ili kwenda kusawazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi
kubwa wa maji haya ya insulin ni kuhifadhi nishati ya mwili kwa matumizi ya
baadae pale mwili unapokuwa una nishati ya kutosha na hautaki kupoteza nishati
ya ziada. Nishati hii huhifadhiwa asilimia kubwa katika mfumo wa glycojeni mwilini mwako kwenye
misuli,ini nk. Sasa inapotokea kiwango chako cha ulaji wa vyakula vya sukari ni
kikubwa sana ndivyo kiwango kingi cha insulin kitatengenezwa na kumwagwa kwenye
mzunguko wa damu kwenye kuhifadhi sukari ya ziada ambayo haitumiki wakati ule
na hatimaye kusazisha kiwango cha sukari mwilini mwako. Kazi ya insulin sio
kushusha sukari kama wengi tunavyofundishwa darasani! Kwa nini nasema hivi?
Kazi ya insulin ni kuhifadhi nishati ya ziada kwa matumizi ya baadae na hivyo
basi kupungua kwa sukari ni matokeo ya kazi ya insulin mwilini mwako.
HEBU SOMA TAFAKURI HII:
Umeingia katika chumba ambacho umekuta
harufu mbaya sana ya deodorant spray au perfume punde tu utakapo ingia katika
chumba hicho utasumbuka sana na harufu hio kwa muda mfupi na hatimaye unaizoea
na kuona ni harufu ambayo haina madhara wala usumbufu kwako.
Huu mfano utakusaidia kujua kwa nini
tunasema insulin yako imeshindwa kufanya kazi, na umepata kizuizi katika
utendaji kazi wake. Nimesema insulin hutolewa kwa kiwango kikubwa sana
kulingana na kiwango cha sukari mwilini mwako, kiwango hiki kingi cha insulin
kwenye damu kwa muda mrefu inaweza kupelekea insulin kupoteza kazi yake
kiuhalisia. Na pia kitu kingine ambacho kinaweza kupelekea insulin kutofanya
kazi ni vipokea insulin kutoitikia kwa sababu ya mafuta mabaya kuleta kizuizi
katika vipokezi vya insulin. Vitendo vyote hivi viwili vinasababisha kiwango
cha insulin kuwa juu wakati wote na kama
nilivyo eleza mwanzo kuwa kiwango cha insulin kinavyozidi kuwa kingi mwilini
mwako kinashusha vichocheo vya Testosterone ambavyo ndio silaha yako mwanaume.
Hivyo basi ukiangalia katika maelezo haya utagundua kuwa ulaji wa vyakula na
vinywaji vingi vya sukari vinasababisha kiwango cha insulin kuwa juu muda wote
ambapo nacho kinapelekea vichocheo vya kiume kushuka na hatimaye unakumbwa na matatizo
ya kukosa matamanio kwa jinsia tofauti,msongo wa mawazo,misuli kukosa nguvu
muda wote umechoka,uzito kuongezeka kwa kasi sanana wengine hupelekea kumilki
vitambi.
Pia kiwango kingi cha insulin kwa muda
mrefu kwenye damu kinaweza kupelekea kupata nywele usoni kwa wanawake,mwanaume
kuishiwa vinyweleo sehemu kama kifuani,tumboni na maeneo mengine mengi.
3.
LEPTINI
Hiki ni kichocheo cha pekee sana na huwa
napenda sana kukizungumzia kwani kinaonesha jinsi gani binadamu alivyo umbwa
kwa kutumia teknolojia ya uhandisi wa hali ya juu. Hiki ni kichecheo ambacho
kinatengenezwa na seli zinazohifadhi mafuta ambazo zinapatikana kwa wingi
kwenye misuli kazi yake kubwa ni kupeleka ujumbe kwenye ubongo katika kuendesha
hamu yako unapokuwa una chakula mbele yako, na ubongo huitikia kwa kutoa
taarifa ya kutosheka na chakula kwa kujihsi umeshiba na huwezi tena kuendelea
na chakula.
Sasa basi ulaji wa vyakula vingi bila
mpango vyenye sukari nyingi unasababisha seli za kuhifadhi mafuta (FAT CELLS)
kutengeneza kwa wingi leptin ili kwenda kutimiza kazi yake. Kiwango cha insulin
na leptin hupanda kwa pamoja kama mapacha vile. Hivyo hivyo kumbuka tafakuri
ile pale juu ya perfume, itafikia wakati kiwango kingi sana kinasababisha
leptin kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ( KUKATA HAMU YA CHAKULA) hivyo
utakuwa una tatizo la kula mlo mkubwa ambao hata siku moja hautosheki na ukitosheka
muda si mrefu unahitaji tena kula. Hawa ndio watu wengi ni wahanga wa muda wote
wanapenda kula vyakula vitamu vitamu tu, hamu haiishi (Sugary addicted,sugar
craving) na wengi huishia kupata matitizo ya kiafya kama kuishiwa nguvu za
kiume,uzito kupita kiasi,kitambi na kuishiwa nguvu kabisa ya misuli yote haya
ni kwa sababu kiwango kingi cha leptin na insulin kinashusha vicheo vyako vya testosterone.
4.
CORTISOL
Hiki ni kichocheo ambacho hutolewa na mwili
pale unapokuwa katika hali yoyote ya mstuko ili kwenda kukabiliana na mtuko
huo.
Mfano labda Dr Boaz Mkumbo nilikuwa
natembea njiani ghafla nikaona nyoka huyo mkubwa chatu. Mwili utastuka sana na
kutoa vichecheo vinavyo enda kupambana na hio hali iliyoshtua mwili wako, mfano
cortisol huenda kuongeza kiwango cha nishati ya mwili (glucose) kwenye damu na
kuwa na nguvu ajabu ya kumkimbia adui yako aliyepo ,mbele yako.
Cortisol pia hutolewa hata kama mwili wako
umekabiliwa na mstuko ndani kwa ndani mfano,sukari mwilini imepungua mwili
unatoa cortisol ambayo kazi yake kubwa ni kubadili ile nishati iliyokuwa
imehifadhiwa katika mfumo wa glycogen kwenye misuli na ini kuwa sukari na
hatimaye kuongeza sukari mwilini mwako.
Sasa tafiti zinasema kwamba,kiwango kingi
cha cortisol kwenye damu kinachosababishwa na msongo,mstuko ndani ya miili yetu
inayo endelea inasababisha LEPTIN kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi yake ipasavyo.
Na endapo leptin ikishindwa kufanya kazi
yake ipasavyo utakuwa una tatizo la kula sana hasa vyakula na vinywaji vya sukari bila hamu kukata na hatimaye
kusababisha insulin kupanda juu na testosterone kushuka chini na hatimaye
kuishiwa nguvu za kiume,matamanio kwa jinsia tofauti nk.
Hongera sana kwa kuendelea kusoma Makala hii,
hapo juu nilitaka kukueleza tu nini kinatokea endapo unapatwa na upungufu wa
nguvu za kiume kwani wengi mmekuwa mkinipigia simu kutaka kujua kwa nini nguvu
za kiume sasa, basi leo nazani umejifunza kitu, kama hujaungana nami katika
ukurasa wangu facebook hebu bofya like Dr Boaz Mkumbo MD utafurahia Makala zangu
nyingi sana nzuri zimeandaliwa kwa ajili yako.
Basi napenda nikupe vitu vikuu 4 vinavyo angamiza
watu kukosa nguvu za kiume hawa ndio maadui wako wakuu kuhusu tatizo lako hilo
mpendwa, hebu endelea kusoma upate suluhisho lako,ufurahie ndoa yako,
VITU 4 VINAVYO ANGAMIZA NGUVU ZAKO ZA KIUME NA KUKUACHA MWENYE MSONGO WA MAWAZO NA MPWEKE KATIKA MAHUSIANO AU NDOA YAKO
Hebu basi napenda nikwambie hawa maadui
wako, najua utashangaa kuwa ni maadui ambao kila siku ni marafiki zako, na
hujui kuwa wanaangamiza msingi wa ndoa yako na inaweza kuwa unajua lakini
unayapuuzia haya tunayokufundisha kupitia elimu hii ya afya, huwa napenda
kuwaambia wagonjwa wangu kuwa afya yako ni mali yako sio ya daktari wala
muuguzi wewe ndiye una mamlaka ya afya yako kuiweka sawa au kuidhoofisha. Hivyo napenda kukuambia kuwa afya yako sio
hazina ya milele linda sana afya kuliko vyovyote ulindavyo kwani ndio msingi wa
furaha zote duniani.
No comments:
Post a Comment