Unapotembea sehemu mbalimbali utagundua kuwa kila nyumba nzuri
yenye thamani imezungushiwa uzio, na uzio unaendana na thamani ya nyumba
na vilivyomo. Utakuta nyingine uzio mrefu huwezi hata kuona miti
iliyopo ndani na nyingine zipo wazi mtu yeyote anapita na kutoka kama
anavyopenda. Vivyo hivyo ukiithamini ndoa yako utaiwekea mipaka, mipaka
ambayo hakuna anayeweza kuivuka. Hapa simaanishi kumuwekea mwenzi wako
mipaka, bali kuiwekea ndoa yako au mahusiano yenu mipaka. Kila mwanandoa au mtu aliyepo kwenye mahusiano lazima ajiwekee
mipaka. Mipaka hii itaiponya ndoa/uhusiano na wale wanaotaka ku tracepass na wewe
itakusaidia pia kukulinda.
Wewe umeoa/ kuolewa ni kwanini basi unaruhusu mtu wa jinsia nyingine
unayemuita rafiki yako akuzoee hadi kuvuka mipaka? Anakuwa huru
kukushika na kukutania utani usiofaa na wewe unachekelea tu? Unakuta
wafanyakazi ofisini wanashikana shikana na kutaniana na wapo kwenye
ndoa, je huoni kama unaruhusu watu watracepass kwenye ndoa yako? Wengine
hata kwenda lunch hawawezi bila dada au kaka fulani na wakati wapo
kwenye ndoa.
Unapokuwa online unachat je umejiwekea mipaka? Message zako na jinsi
unavyochat na watu umeweka mipaka? Watu wamejikuta wanatoka nje ya ndoa
sababu ya ku entertain chat zisizofaa na hadi wanajikuta emotionally
connected na mtu asiye mwenzi wake. Unafika nyumbani busy na simu na
hata mwenzi wako huna muda naye tena maana tayari kuna mtu umeconnect
naye emotionally kupitia simu.
Je ndugu wanaweza ingilia maamuzi yenu na kuyabadilisha bila nyie
kuwasiliana? Ni nafasi gani wazazi wanayo kwenye ndoa yenu maana hapa
pia panahitaji mipaka. Wazazi ni walezi na washauri lakini wenye maamuzi
ni mume na mke.
Weka mipaka kwenye ndoa yako, tena mipaka inayostahili maana ndoa ina thamani kubwa.
Chazo: Docta Joh Blog




No comments:
Post a Comment