Baada
ya kusoma makala inayohusu kijana mmoja aliyesumbuliwa na kwikwi kwa
zaidi ya miaka miwili na nusu, na baadaye kutibiwa tatizo hilo kwa
kufanyiwa upasuaji wa ubongo na kutolewa tezi, nimeamua leo nizungumzie
kwikwi.
Kwiki ni kitendo kisichozuilika ambacho hutokana na kusinyaa kwa kuta za iwambo cha moyo au diaphragm. Kwa kawaida kwikwi ni kitendo kinachojirudia rudia mara nyingi. Sauti ya 'hic' inayotokea wakati unapokuwa na kwikwi husababishwa na kidaka tonge (epiglottis) ambacho hufunga haraka wakati hewa inapoingia kwenye koo. Kupiga kwikwi kwa kawaida hakuna maumivu lakini mara nyingine husumbua hasa inapoendelea kwa muda mrefu. Kwikwi ya kawaida huweza kutulizwa kwa kunywa maji, lakini wakati mwingine kufanya hivyo hakusaidii.
Zifutazo ni sababu zinazoweza kukuletea kwikwi
1. Kula kwa haraka.
2. Kula chakula cha moto na kunywa maji baridi baada yake.
3. Kulia au kukasirika.
4. Kula chakula chenye viungo vingi au pilipili.
5. Kula chakula cha moto sana.
6. Kunywa pombe au soda kwa wingi.
7. Kukohoa sana.
8. Kucheka kupita kiasi.
9. Kufurahi sana, kusisimka au kupatwa na msituko.
1. Kula kwa haraka.
2. Kula chakula cha moto na kunywa maji baridi baada yake.
3. Kulia au kukasirika.
4. Kula chakula chenye viungo vingi au pilipili.
5. Kula chakula cha moto sana.
6. Kunywa pombe au soda kwa wingi.
7. Kukohoa sana.
8. Kucheka kupita kiasi.
9. Kufurahi sana, kusisimka au kupatwa na msituko.
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa,
vitu ambavyo vinakiletea karaha kiwambo cha moyo au diaphragm
husababisha kwikwi. Kuna sababu nyingi ambazo husababisha jambo hilo na
hizo tulizotaja hapo juu ni miongoni mwazo,ambapo matokeo yake ni
humfanya mtu apige kwikwi. Kwikwi kwa kawaida
huisha baada ya dakika chache au hata sekunde. Lakini iwapo kwikwi
itaendelea kwa masaa au kwa siku, huweza kuwa ni tatizo muhimu la kitiba
na pengine hali kama hiyo inaweza ikawa inasababiswa na ugonjwa.
Kuna baadhi ya watu hupata kwikwi
sana wakati wa ujauzito, baada ya kufanyiwa operesheni na hata watoto
wachanga pia hupatwa na kwikwi mara kwa mara. Wajawazito hupata kwikwi
sana mwishoni mwa miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito na mwanzoni mwa
miezi mitatu ya pili. Kwikwi hutokea wakati wa ujauzito ni kwa sababu
wakati huo uwezo wa
kuvuta hewa ndani ya mapafu na
kutoa nje huongezeka kwa asilimia 30 hadi 40 ikilinganishwa na hali ya
kawaida. Hakuna sababu inayojulikana inayosababisha kwikwi kwa watoto
wachanga, na wazazi wanashauriwa wasitiwe hofu na suala hilo. Hii ni
katika hali ambayo kwikwi baada ya upasuaji husababishwa na nusu kaputi
au anesthesia.




No comments:
Post a Comment