HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » FAHAMU ZAIDI KUHUSU UGONJWA WA GOUT

 Gout ni aina ya ugonjwa wa arthrits ambao anaambatana na maumivu makali kwenye joint, kuvimba kutokana na mrundikano wa uric asidi ambayo hujikusanya na kufanya kama jiwe gumu kwenye joint. Hapo zamani gout ulijulikana kama ugonjwa wa wafalme (a disease of Kings) kutokana na unywaji wao wa pombe na vyakula vya kukidhi raha zao. Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza ni mmoja ya wafalme waliougua ugonjwa huu. Alexander the great, Christopher columbus, Sir Isaack newton ni baadhi ya watu maarufu ambao waliugua ugonjwa wa Gout.kibaya zaidi ni kwamba namba ya watu wanaougua ugonjwa huu kwa sasa inaongeza taratibu haijalishi unatoka familia ya kitajiri ama laa.
GOUT NI NINI HASA
Huu ndio ugonjwa wa joints ambao huwashambulia sana na kuwapa maumivu makali wanaume. Wanawake pia huweza kuathirika na ugonjwa huu hasa baada ya kukoma hedhi. Ugonjwa huu huleta maumivu makali ya ghafla, hasa kwenye sehemu linapoanzia dole gumba la mguu. Dalili za ugonjwa huanza kuonekana pale uric acid, tindikali ambayo huzalishwa na mwili katika ufanyaji kazi wake (ambayo haina manufaa kwa mwili) hubakia katika viungo vya mwili na katika majimaji ya mwili. Uric acid iliyoganda (tophi) huweza kujikusanya na kubaki chini ya ngozi inayozunguka joints, huweza pia kujikusanya ndani ya figo na kusababisha kidney stones (namna ya kokoto ndogo ndani ya figo)
Gout inaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye maungio ya mifupa na figo. Endapo hatua za kuutibu ugonjwa huu hazitachukuliwa kwa muda mrefu (miaka 10 au zaidi), madhara ya kudumu humtokea mgonjwa
Chanzo Cha Gout Ni Nini?
 Gout kutokea kimsingi pale tindikali aina ya uric (uric acid) inapozidi kiwango katika mwili wa binadamu hali ambayo kiutaalamu huitwa hyperuricemia. Tindikali hii ni matokeo ya kuvunjwavunjwa na mwili kwa aina fulani za chakula kama nyama, nyama ya kuku na chakula cha baharini. Tindikali hii kwa kawaida huchanganyika na damu na mwisho hutolewa nje ya mwili pamoja na mkojo kupitia figo. Tindikali hii ikitengenezwa kwa wingi mno au isipotolewa nje ya mwili kwa kiwango kinachosatahili, ile inayobakia huganda na kukaa kwenye maeneo ya joints na kusababisha maumivu kwenye joints hizo na maeneo yaliyo karibu. Kuna mazingira ambayo hupelekea hali hii ya uzidifu wa tindikali ya uric katika mwili na mwishowe gout kutokea nayo ni:
·         Jinsia: Wanaume huzalisha tindikali ya uric kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wanawake, viwango vya uzalishaji kwa wanawake vikikaribia vile vya wanaume pale tu wanapokoma hedhi.
·         Urithi: Kuzaliwa kwenye familia yenye historia ya gout kunakufanya uwe kwenye hatari kubwa zaidi ya kuupata ugonjwa huu.
·         Mtindo wa maisha: Unywaji wa pombe huzuia utolewaji wa uric acid   nje ya mwili na ulaji wa chakula chenye purine kwa wing  husababisha kiwango cha tindikali ya uric kuwa kikubwa mwilini.
·         Madini ya lead: Kuwa karibu na madini haya kwa muda mrefu  kumeonyesha kuhusika na aina fulani za gout.
·         Madawa: Baadhi a madawa yameonekana kuongeza kiwango cha uric acid mwilini.
·         Unene: Unene umedhihirika kuongeza hatari ya kupatwa na gout.
·         Matatizo ya kiafya: Kama figo hazifanyi kazi vizuri kiwango cha  uric acid mwilini kitapanda. Matatizo mengine ya kiafya  yanayochangia ni high blood pressure (hypertension), kisukari na  hypothyroidism.
DALILI ZA GOUT
Ugonjwa wa gout huanza ghafla na mara nyingi katikati ya  usiku. Ugonjwa huanza kwa kuleta maumivu makali kwenye maungio ya mifupa na mara nyingine kuambatana na uvimbe. Gout mara nyingi hushambulia maungio makubwa ya dole gumba la mguu lakini pia huweza kushambulia maungio ya mikono, ankles, viwiko vya mikono na vidole.

 TIBA YA GOUT

Matatizo yaliyo mengi ya gout huondolewa kwa kutumia dawa dawa nzuri ya gout ni Allupurinol pia Nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama brufen , colchicine au corticosteroids hutumika kuondoa maumivu kwenye eneo lililoathirika na gout,
Upande wa pili ni dawa za asili zinafanya vizuri sana katika kutibu tatizo hili bila kukuletea madhara kwenye mwili. Ila hakikisha tu unatafuta kituo sahihi chenye dawa zenye ubora mkubwa. Mtindo wa maisha unaweza kusaidia katika kupunguza makali ya ugonjwa huu au kuzuia usikupate. Yafaa kufanya yafuatayo:
– Kunywa maji mengi, lita 2-4 kwa siku
– Kutokunywa pombe
– Kuweka uzito wa mwili kwenye kiwango kinachofaa
– Kupata mlo uliokamilika (balanced diet)
– Kutotumia vyakula vyenye purines kwa wingi (vinavyozalisha uric acid kwa wingi). Vyakula vya kula kwa kiasi kidogo ni maharage na njegele zilizokaushwa, nyama pori, uyoga na maini.

Pia kuna dawa za hospitali maalumu kwa ajili ya tatizo hili,bas ni muhimu kufika hospitali uonapo hizi dalili.


IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: