watu wengi huona nta iliyopo sikioni kama uchafu hivyo hujijengea tabia
ya
kuiondoa mara kwa mara bila kujua kuwa huwa na kazi muhimu ndani ya sikio.
Mtaalamu
huyo alisema kuwa, nta ina kazi nyingi. Kazi hizo ni kama vile kuzuia
vijidudu vya magonjwa visiathiri sehemu ya ndani ya sikio, kuzuia
vumbi,
kulainisha ngozi ya ndani ya sikio na kuhusika katika kuchuja sauti sambamba na viungo vingine vilivyopo ndani ya sikio.
Kutokana na faida hizo, endapo mtu atakuwa na tabia ya kuiondoa nta kila
mara, tena kwa kutumia vijiti vya pamba ‘pamba stick,’ huwa katika
hatari ya kukosa faida zilizoainishwa hapo awali na kujisababishia
madhara kama vile muwasho ndani ya sikio (itching) kutokana na bakteria
wa fangasi na vumbi ambalo litakuwa likiingia bila kizuizi.
Hatari ya pili ni kukauka kwa ngozi ya ndani ya sikio na maumivu makali
hasa kama mtu huyo atakuwa katika mazingira yenye kelele nyingi na
mwisho kabisa ni kuharibika kwa ngoma ya sikio na mfumo mzima wa
usikivu.
Hata hivyo, pamoja na faida hizo za nta ndani ya sikio ni vyema mtu
akajua kwamba nta ikizidi sikioni huweza kusababisha kuziba kwa sikio,
kusababisha kizunguzungu na kuhisi karaha (discomfort) hivyo ni vyema
kama mtu atakuwa
akiondoa nta hiyo angalau mara moja kwa kila miezi miwili kwa afya yake.
“Nta huwa uchafu kama itazidi sikioni ni vyema kujiwekea ratiba ya
kuondoa kila baada ya miezi miwili kuliko kufanya hivyo kila mara,”
alisema Dr. Bujiku.
IMEANDALIWA NA DOCTOR JOH BLOG
No comments:
Post a Comment