Muda gani mzuri wa kupima mimba ni upi?
Unapotaka kubeba mimba au unapokua na wasiwasi kwamba umepata mimba,
mara nyingi hua ni changamoto kwa wasichana kwani wengi wao hujikuta
wanapima siku hiyohoyo au kesho yake kuangalia kama mimba imeingia kitu
ambacho hata kwa vipimo vya kisasa zaidi huwezi kupata majibi sahihi kwa
muda mfupi hivyo.
Muda mzuri wa kupima mimba kwa uhakika zaidi ni pale unapokosa siku zako
za hatari za mwezi unaofuata, kipindi hiki zile homoni ambazo kitaalamu
ndio zinasomwa kwenye mkojo mtu akiwa na mimba kwa jina la human
chorionic gonadotrophin hormone zinakua tayari ziko za kutosha hata kwa
vile vipimo ambavyo havina nguvu sana vinasoma kwa uhakika.
Muda unaotumika kwa kipimo kusoma inatofautiana kwa wanawake tofauti..
Wakati unataka kupima mimba unatakiwa ujue kwamba wanawake
wanatofautiana sana wao kwa wao kutokana na urefu wa mizunguko yao yaani
wengine mizunguko mirefu na wengine mfupi.
yai la mwanamke na mbegu ya mwanaume vinapokutana huchukua siku saba
mpaka kumi kuweza kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi, baada ya
hapo baada ya siku mbili mpaka tatu ndio mimba inaweza kusoma...
Hivyo
kwa ujumla tunasema inaweza kuchukua siku 14 mpaka siku 21 kusoma
kama mimba imeingia au haijaingia baada ya kulala na mwanaume. wanawake
wengine hutokwa na damu kidogo mimba inapojishikisha kwenye ukuta wa
uzazi kitaalamu tunaita implantation bleeding, damu hii hua inakua
kidogo sana kuliko ile ya kawaida ya hedhi lakini kipindi hiki mimba
inakua bado haijasoma kwenye kipimo.
Unatakiwa upime saa ngapi?
Kila unavyopima kipimo cha mkojo, unakua unapima homoni ya human chorionic gonadotrophin hormone ambayo nimeitaja hapo juu.
Muda mzuri ambayo homoni hiyo inaonekana ni asubuhi, hivyo zingatia
kupima mimba asubuhi kwa majibu mazuri zaidi, wakati mwingine ukipima
mchana unaweza kuona mistari ambayo inafifia yaani haina rangi nyekundu
ya kutosha.
No comments:
Post a Comment