Madaktari
wakiwa kazini kuhakikisha wanaokoa maisha ya mtoto huyo.
Inasikitisha sana kwa mtoto wa miaka minne kufanyiwa kitendo kibaya na baba yake mzazi
Afande Bwire
akiwa na pingu zake wodini
KAHAMA
Mkazi
wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa
Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa
kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa
kimapenzi.Endelea kupitia mtandao huu ili upate habar zaidi.Tukio
hilo limetokea jana jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana
na mke wake Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe
alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza
kumkata mapanga kichwani.
Kwa
mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba
walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona
aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga
mlango.
Imefafanuliwa
kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja
milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika
walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za
kichwani.Majirani
kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa
cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi
kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.
Hata
hivyo Wakati gari la Polisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la
Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami
kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.
Mtoto
Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya
Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.na
mwanaafrika
No comments:
Post a Comment