Thursday, June 20, 2013

JESHI LA POLISI SONGEA LAKAMATA MENO 18 TEMBO NA NOTI BANDIA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deudedit Nsimeki akiwa ameshika noti za bandia ambazo zilikamatwa wakati wa kuuza mahindi katika soko la Sodeko Manispaa ya Songea
Haya  ndio meno ya tembo ambayo yamekamatwa katika kijijicha Hanga yakiwa meno 18 ambayo yalikuwa yakisafirishwa kwenda Dar es salaam
Kweli watu  hawana huruma hayo ni meno ya tembo wadogo ambao walikuwa wakitegemewa kuwa watakuwa rasilimali ya taifa lakini masikini wawindaji haramu wamekatisha maisha ya tembo hao
Noti bandia zilizokamatwa Manispaa ya Songea katika soko la Sodeko, kwa mujibu wa kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma 
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata Vipande 18 vya Meno ya Tembo vikiwa kwenye Mfuko wa Salfeti. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amefanikisha kukamatwa kwa meno ya Tembo vipande 18 vikiwa kwenye Mfuko wa Salfeti maeneo ya Hanga Misheni wilaya ya Namtumbo


PICHA NA SONGEA HABARI

WABUNGE WA CHADEMA WASIMULIA MKONG'OTO


Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu akiwaonyesha waandishi wa habari miwani yake aliyodai kuvunjiwa na polisi. Lissu alipata dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati, jijini Arusha jana baada ya kukamatwa juzi. Picha na Moses Mashalla 

Arusha/Dar es Salaam. Wabunge wanne wa Chadema, ambao waliachiwa na polisi kwa dhamana wamesimulia mateso waliyoyapata wakiwa rumande baada ya kukamatwa juzi.
Vigogo hao; Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti maalumu), walikamatwa juzi baada ya wao na wafuasi wa chama hicho kutawanywa kwa mabomu ya machozi na polisi kwenye Viwanja vya Soweto, Arusha.
Wabunge hao waliachiwa baada ya kujidhamini wenyewe huku watu wengine 65 waliokamatwa pamoja nao wakiachiwa baada ya kudhaminiwa.
Wote wanatakiwa kuripoti kwenye kituo hicho Julai 22, mwaka huu na wataelezwa hatma ya suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi lake linaendelea kuwasaka Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema na kuwaonya kuwa wanatakiwa kujisalimisha mara moja.
Chagonja alisema Mbowe na Lema wanatafutwa kwa kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali katika viwanja hivyo vya Soweto walipokuwa wakitaka kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki dunia baada ya kuumizwa kutokana na mlipuko wa bomu, Jumamosi iliyopita.
Pia aliwaamuru Mbowe na Lema kuwasilisha mara moja ushahidi wa kuwahusisha polisi na shambulio la bomu na kama hawana imani na Polisi, basi wawasilishe ushahidi wao kwa Rais Jakaya Kikwete.
Lissu
Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alilalamikia kitendo cha polisi kumwagia maji ya kuwasha baada ya kumkamata.
“Walinimwagia maji ya kuwasha kwa mfululizo nikalazimika kulala chini kifudifudi huku nikiwa nimefunika macho kukwepa yasiingie maji. “Kuna askari walitaka kunipiga lakini niliokolewa na mwenzao mmoja aliyenikinga nisishambuliwe. Kwa kweli ilikuwa hali ya hatari,” alisema.

WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WABEBESHWA MZIGO WA UALIMU WA SAYANSI ROMBO


 Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Nduweni Sekondari, Venance Mramba.
 Baadhi ya wanafunzi Sekondari ya Nduweni wakiwa darasani
Baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Urauri, Wilaya ya Rombo.
Sehemu ya maktaba ya Sekondari ya Tanya, ikionesha utitiri wa vitabu vya sayansi japokuwa haina walimu wa somo hilo.

MOSHI, Tanzania
KITENDO cha upungufu wa walimu wa sayansi nchini hasa katika shule za sekondari zinazomilikiwa na serikali kimezidi kuibua changamoto maeneo mbalimbali nchi. Shule ambazo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa ni sekondari za kata ambazo uwingi wake umechochea zaidi changamoto hiyo.

Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo ambayo yanakabiliwa na changamoto hiyo ya uhaba wa walimu wa sayansi kama ilivyo kwa mikoa tofauti ya Tanzania. Hata hivyo walimu wakuu wa shule zenye changamoto wamebuni mbinu mbadala kukabiliana na hali hiyo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JUNE 20,2013









Wednesday, June 19, 2013

MSIKILIZE HAPA ALICHOKISEMA SAIDA KAROLI BAADA YA KUZUSHIWA KUWA AMEFARIKI DUNIA

 

SIKILIZA SAUTI HAPA SAUTI YAKE

SHINDANO LA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2013 LAZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM


 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2013, akifafanua jambo wsakati wa uzinduzi wa shindano hilo. (Picha zote Habari Mseto Blog)
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam. 
 Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search jijini Dar es Salaam leo.


SHINDANO la Epiq Bongo Star Search linatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 29 mwaka huu huku likiwashilikisha wadau wakubwa wa muziki hapa nchini kwa lengo la kuwajenga washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi utakaowasaidia kukua kimuziki.

Akizungumza katika makao makuu ya Kampuni ya simu za Mkononi ya Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen alisema, shindano hilo linatarajiwa kufanyika usajili katika Mikoa Sita ambayo ni Mwanza, Mbeya, Arusha, Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam.

Rita alisema, Mwaka huu kauli mbiu ‘Kamua’ na kudai kuwa wamejipanga kuwafikia vijana wengi hapa nchini, na pia kutengeneza nyota wengi wa muziki mbali na mshindi na kudai kuwa wataanzia Mkoani Dodoma Juni 29-30, katika ukumbi wa Maisha klabu, Julai 5-6 Zanziba Hotel ya Bwawani, Mbeya Julai 10-11 Klabu Vybes, Mwanza Julai 14-15 Klabu Fassion, Arusha Julai 20-21 Tripple A na kumalizia Dar es Salaam Julai 26-28 uwanja wa Taifa.

Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema, Zantel wanajivunia kufanya kitu kikubwa kama hiki ambacho kinawapatia vijana ajila, na kudai kuwa, wanatarajia kufungua laini ya kurekodi kwa simu kuanzia siku ya kwanza ya usaili Mikoani ambapo washiriki watapiga namba 0901551000 au kutuma neno Kamua kwenda 15530.

Epiq BSS, imekuwa ikiwatoa vijana katika hali ya umasiki na kuwapa ajili kama ilivyo kwa wasanii kama Kala Jeremaya ambaye anatikisa katika muziki wa Hiphop pamoja na Walter Chilambo aliyetwaa taji hilo mwaka jana.

KIPANYA LEO JUMATANO


NJAA YATOROSHA WANAFUNZI SHULENI


Wanafunzi wakinunua vitafunwa

Ukosefu wa chakula cha mchana katika Shule ya Sekondari Kimochi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro chanzo cha baadhi ya wanafunzi kukithiri kwa utoro kutokana na njaa wakati wa masomo nyakati za jioni.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo, Karimu Msangi, tatizo hilo linatokana na wazazi kutochangia fedha kwa ajili ya kunua chakula kwa ajili ya mlo huo kusabaisha kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo.
Alisema utoro na  matumizi ya dawa za kulevya kwa baadhi ya wanafunzi kumesababisha  matokeo ya mitihani ikiwamo ya kitaifa kuwa mabaya na kushuka kwa kiwango cha elimu shuleni hapo. 

“Watoto hawapati chakula cha mchana na wakati mwingine hata majumbani walipotoka hawakupata kifungua kinywa ni vigumu kumfundisha mwanafunzi wa aina hii na pia ni vigumu kupata matokeo mazuri kitaaluma... wazazi wamekuwa ni wagumu sana katika kuchangia, ”alisema Msangi
Msangi aliongeza kuwa katika uchunguzi wake amebaini kuwa wanafunzi wengi wanaporuhusiwa kurudi nyumbani,  wanaishia kuzurura mitaani na wengine kujiingiza katika makundi ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimochi,  Samweli Meta aliliambia NIPASHE kuwa  uongozi wa kijiji umejipanga kuwafuatilia wazazi hao na kurudisha utaratibu wa wanafunzi kupata mlo wa mchana shule zitakapofunguliwa ili waendelee na masomo.
Diwani wa Kata ya Kimochi, Ananyisa Macha  aliwataka wazazi  ambao hawajalipa michango mbalimbali shuleni hapo kuwasilisha kabla ya Agosti mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.
CHANZO: NIPASHE

YALIYOJIRI KWA PICHA KWENYE VURUGU ZA HUKO ARUSHA HAPO JANA JIONI










PICHA LEO: KWELI MTOTO KWA BABA HAKUI MTIZAME BABA YAKE BILL GATETS MWENYE MAKA 87 AKIWA NA MWANAE


Mzee William H. Gates, Sr. baba yake Bill Gates 

OXFAM KWA KUPITIA KAMPENI YA GROW YATOA WITO KWA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KWA WAKULIMA WADOGO NA WA KATI.

 Mwanasheria –Mshauri Mwelekezi katika Masuala ya Haki za Ardhi – Emmanuel Massawe akifafanua jambo kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwatangaza rasmi mabalozi wa OXFAM katika Kampeni ya GROW nchini itakayowezesha mfumo wa chakula kuwa wa haki na salama

 Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan akziungumza na wageni waalikwa namna kampeni hiyo itakavyofanya kazi zake za uhamasishaji hapa nchini.
 Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW wakati wa hafla hiyo.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
 Jacob Stephen Muigizaji.
 Masoud Kipanya Mchora Katuni.
 Dina Marious- Mtangazaji wa Redio
 Khadija Mwanamboka – Mbunifu wa Mavazi akipozi na Tuzo yake mara baada ya kutangazwa rasmi.


Shamim Mwasha Fashion Blogger.
Mabalozi wa OXFAM katika kampeni ya GROW katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkazi OXFAM-Justin Morgan (wa pili kushoto).

Na.Mo Blog Team
Taasisi isiyo ya kiserikali ya OXFAM kwa kupitia Kampeni yake ya GROW imewakutanisha pamoja masupa staa saba wa Tanzania wakiwemo Mbunge wa Kawe Mh. Halima Mdee pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Shy-Rose Bhanji kufanyakazi pamoja na vikundi vya wanawake wajasiriamali na wazalishaji, kwa lengo la kuhakikisha hakuna mtanzania atakayeteseka kwa njaa wakati mbinu za kilimo zinaweza kufanikiwa.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha rasmi mabalozi wa OXFAM kupitia kampeni hiyo, mmoja wa mabalozi hao Bi. Khadija Mwanamboka amesema kilimo sio tu ni sekta endelevu nchini Tanzania bali pia ni Nyanja inayowezesha kupatikana kwa chakula kwa familia na akiba ya chakula kwa taifa kwa kuwa asilimia 80 ya wajasiriamali nchini ni wakulima.
Nchini Tanzania takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wajasiriamali wanawake wanajihusisha na kilimo kikiwepo cha mbogamboga na matunda.

Aidha kampeni hiyo inakusudia kuendeleza na kukuza uzalishaji utakaoyafanya mazao hayo ya kilimo kuwa na bei muafaka kwa faida ya wakulima hao wa chini na wa kati.

ARFI, LISSU WATIWA MBARONI ARUSHA


Arusha. Wabunge wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu) wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye Uwanja wa Soweto jana.
Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jana kwamba pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu wapatao 60 kutokana na vurugu zilizozuka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.
Mbali ya viongozi hao, alisema wanawasaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
“Tunawasaka wabunge ili tuwajumuishe na watu hawa kwa kosa la kuhusika na mkusanyiko usiokuwa halali. Hadi sasa tumefanikiwa kulinasa gari la Mbowe,” alisema Chagonja.
Pia kamatakamata hiyo imemkumba Mpigapicha wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Ashraf Bakari. Polisi walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya waombolezaji hao.
Awali, Kamishna Chagonja alisema jana asubuhi kuwa wamelazimika kuzuia viwanja hivyo kutumika baada ya wamiliki wake, AICC kuzuia shughuli za Chadema kwenye eneo lao.
Kamishna Chagonja aliwaonyesha waandishi wa habari barua aliyosema imeandikwa na uongozi wa AICC kuzua Chadema kuendelea kuutumia Uwanja wa Soweto.
Mabomu yarindima
Dalili za kuzuka kwa vurugu zilianza kuonekana asubuhi baada ya polisi kuzingira uwanja huo na kuzuia watu waliokuwa wameanza kufurika katika eneo hilo kuanzia saa moja kuingia kwa ajili ya maombolezo.
Wakati Polisi wakiwa uwanjani, wananchi walijaa nje ya uwanja na kuonekana kama wamewazingira.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe waliwasili uwanja hapo yapata saa nane mchana na kukuta zuio hilo na kuanza kuzungumza na wananchi ingawa FFU walikuwa wakiwataka watu kutawanyika. Mabomu yalianza kurindima wakati Arfi aliposimama na kuwahimiza wananchi kuelekea Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu.
“Tuna muda mfupi sana wa kuzungumza hapa, tunaomba wote tuelekee Hospitali ya Mount Meru kuaga miili ya marehemu kwa sababu uwanja huu umezuiwa na polisi,” alisema Arfi kabla ya kukatishwa na milipuko ya mabomu.
Awali, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema alitoa msimamo wa chama hicho kuwa Mwenyekiti wao, Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wa tukio la bomu wala kujisalimisha polisi kwa sababu hawana imani na jeshi hilo.
“Namtaka Chagonja atangulie mahakamani, tutakutana hukohuko. Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wala kujisalimisha polisi...” alisema Lissu na kuongeza:
“Kisheria haiwezekani polisi ambao ndiyo watuhumiwa ndiyo wadai kukabidhiwa ushahidi ili wauharibu.”
Mapema Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa polisi kuhusika na tukio la kurusha bomu kwenye mkutano wa Chadema la sivyo polisi watatumia sheria kuwalazimisha kufanya hivyo.
Hekaheka
Baada ya polisi kuanza kutupa mabomu saa 8.45 mchana, wabunge, viongozi waandamizi wa Chadema na watu waliokuwa wamekusanyika walilazimika kutimua mbio.
Watu walioshuhudia tukio lile wanasema viongozi hao akiwamo Mbowe na mwenzake Lissu walikimbilia kwenye magari yao. Lema alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe, (kitimoto) kwenye maeneo ya Kaloleni.
Kabla ya polisi kurusha bomu mahali alipokuwapo Lema, mbunge huyo alisikika akisema:
“Jaribuni kuvumilia, tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali cha kuleta miili ya wapendwa wetu hapa, kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wana usalama ambao wanalinda amani, ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wameshakufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshima zote.”
Kauli hiyo iliwachefua polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo na kwamba hakutakuwa na suala la kuaga miili ya watu hao katika eneo hilo. Ghasia hizo zilisababisha kusimama kwa shughuli za biashara na kijamii kwa muda jijini Arusha huku watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na maeneo yalikorushwa mabomu wakilazimika kutoka nje kupata hewa safi baada ya nyumba hizo kujaa hewa ya mabomu.
Polisi waliokuwa wakirusha mabomu waliwakimbiza wananchi hadi maeneo ya Sakina huku wakiendelea kufyatua mabomu kila walipoona mkusanyiko wa watu.
Katika eneo la Kaloleni, mkabala na Ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo baadhi ya wafuasi wa Chadema walichoma matairi barabarani na kusababisha ifungwe. Pia walichoma matairi katika eneo la Mianzini.
Katika eneo la Tanki la Maji, Barabara ya kwenda Moshi, baadhi ya wafuasi wa Chadema walipanga mawe barabarani na kusababisha msongamano wa magari.
Katikati ya jijini Arusha barabara zilikuwa hazipitiki kutokana na nyingine kufungwa na kusababisha usumbufu mkubwa.
Waandishi nao matatani
Katika vurugu hizo, baadhi ya waandishi wa habari walishambuliwa na polisi. Hao ni pamoja na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti dada la The Citizen, Zephania Ubwani ambaye kabla ya kuchomoka katika mikono ya askari, alikuwa akiwaonyesha kitambulisho chake cha kazi.
Hata hivyo, askari hao walimtishia kumtandika na kisha kumwambia aondoke katika eneo hilo kwa kuwa haijalishi yeye ni nani.
Mwingine ni mwandishi wa gazeti la Nipashe, Cnythia Mwilolezi ambaye alilazimika kuacha viatu na vitendea kazi vyake katika Uwanja wa Soweto na kukimbilia kwenye moja ya nyumba zilizopo jirani na eneo la tukio.
Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Moses Kilyinga alipigwa na polisi baada ya kuonekana akichukua maelezo.
Kilyinga ambaye alishambuliwa na askari hao alisema mara baada ya askari hao kumkamata, alijitambulisha lakini hawakumwelewa na wakaendelea kumchapa kabla ya kufanikiwa kuchomoka. 
Polisi wavamia hospitali
Wakati baadhi ya majeruhi wakidai kushuhudia polisi wakiwapiga risasi watu waliokuwa wakimkimbiza mtu aliyerusha bomu katika tukio la Jumamosi, askari hao juzi walifika katika Hospitali ya Seliani saa mbili usiku wakitaka kumchukua mmoja wa majeruhi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa baada ya mgonjwa kutokomea kusikojulikana baada ya kupata taarifa za kutaka kuhusishwa na tukio hilo.
Ingawa si polisi wala Chadema waliokuwa tayari kumtaja mgonjwa huyo, inaelezwa kwamba majeruhi anayesakwa ni Abdallah Alila aliyekaririwa na vyombo vya habari jana na juzi akidai kumshuhudia aliyerusha boma akiondoka kwenye moja ya magari ya polisi.
Hata hivyo, Kamishna Chagonja jana alisema kwamba jeshi lake linapenda kushirikiana na raia kupata taarifa na si kutumia nguvu katika kukusanya ushahidi wake.

MWANANCHI