HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » MAMA MDOGO WA ANETH ANAYEJULIKANA KWA JINA LA BAHATI LUKANGARA AMEFIKISHWA LEO MAHAKAMANI KWA UNYANYASAJI WA MTOTO KWA KUMUUNGUZA VIBAYA MWILI WAKE

 
HUYU NDIYO MAMA MDOGO WA ANETH AMEJULIKANA KWA JINA LA  BAHATI LUKANGARA NDIYO ALIYEMUUNGUZA MTOTO ANETH

MWANAMKE anayetuhumiwa kumnyanyasa mtoto wa dada yake kwa kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto, hatimaye amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shtaka linalomkabili.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Achiles Mulisa ameiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto  Aneth.

Mulisa akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu  cha 222(a) sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.

Kutokana na kosa hilo mshtakiwa amekana shitaka hilo ambapo amerudishwa mahabusu hadi Novemba 22, Mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Mwendesha mashtaka huyo alisema Mshakiwa amenyimwa dhamana kutokana na hali ya mhanga ambaye ni mtoto Aneth kutokuwa ya kuridhisha na kuongeza kuwa sababu nyingine ni kwa ajili ya usalama wake.

Alisema upande wa Jamhuri unamashahidi wanne ambao wataanza kutoa ushahidi wake mahakamani hapo Novemba 22, Mwaka huu kutokana na upelezi kukamilika.

Aliwataja mashahidi hao kuwa ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru Mwakanyamale, Daktari anayemtibu mhanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul.

Wengine ni Askari Polisi aliyepeleleza kesi hiyo WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao wako tayari kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.

Awali mshatakiwa huyo aliieleza mahakama kuwa na uhusiano na mtoto  huyo ambapo pia alikiri kuwa na taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo na kuhusu kukatwa kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP) kwenye mkono uliobaki.

  Kwa Hisani ya Venance Matinya,

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: