HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » Hii inawahusu Simba na Yanga: Kikwete kuzindua Azam Complex

Rais Jakaya Kikwete 
Rais Jakaya Kikwete, leo mchana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Uwanja wa Azam Complex unaomilikiwa na klabu ya Azam FC, Chamazi, Mbande, Dar es Salaam.

Kikwete atazindua uwanja huo ambao tayari ulishaanza kutumika kwa mechi za Ligi Kuu Bara na michezo mingine tangu msimu wa mwaka 2011 chini ya Mkurugenzi Mkuu, Aboubakary Bahkresa.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Idrissa Nassor aliliambia gazeti hili kwamba pamoja na uwanja huo kuanza kutumika tangu mwaka 2011, lakini ulikuwa bado haujazinduliwa rasmi.
“Kweli Rais (Kikwete) atakuwa mgeni wetu kwenye uzinduzi wa uwanja wetu. Ni mara ya kwanz utakuwa ukizinduliwa tangu ulipoanza kutumika mwaka juzi,” alisema Nassor.

Azam inayoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrka, imekuwa ikicheza mechi zake zote za Ligi Kuu kwenye uwanja huo kwa kipindi chote kabla ya uzinduzi.

“Tumecheza mechi zote za ligi kwenye uwanja huu, isipokuwa mechi dhidi ya Simba na Yanga ambazo tumekuwa tukicheza Uwanja wa Taifa kutokana na uzito wa mechi,” alisema Nassor.

Klabu ya Azam ndiyo pekee Tanzania inayomiliki uwanja wa soka wa kisasa licha ya kuwa imeanzishwa chini ya miaka 10 iliyopita na kuzishinda za Simba na Yanga.


MWANANCHI

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: