HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » AFANDE SELE: NIKIISHI DAR KWA KIPATO CHANGU NTAPATA TABU SANA, SIHAMI MORO


Usitarajie kabisa kumuona Seleman Msindi aka Afande Sele akihamia Dar es Salaam. Akiongea na safu ya Starehe ya gazeti la Mwananchi, Mfalme huyo wa rhymes ambaye tangu aanze muziki hajawahi kuhamisha makazi yake kutoka Morogoro, amesema jiji la Dar haliwezi, kutokana na kuwa na maisha ya juu. 

“Dar kunaongeza matumizi,” alisema Afande. “Kwa kipato changu nikiishi huko nitapata tabu, kwa kuwa wasanii karibu wote wanakutana katika nyumba ya starehe kitu ambacho kinahitaji fedha, ni wachache sana ambao wanakubali kushindwa kwa kukaa nyumbani baada ya shoo, sasa kwa kuwa napenda kujichanganya na kubadilishana mawazo na wenzangu sintoweza kukaa nyumbani nitakwenda nao viwanjani hayo ndiyo mambo nisiyoyataka.
Ninaamini vijana wengi wanashindwa kufikia malengo yao kutokana na kuendekeza anasa zinazopatikana huko, bila kujali wapo na wasanii gani, kuna wengine wakubwa na wanapata fedha nyingi sasa bila kujua wengine wanajiingiza katika matumizi na kujikuta wakiishia kuvaa na kufanya starehe tu.”
Wakati huo huo, Afande amelazwa hospitali kwa siku tatu leo kutokana na kusumbuliwa na Malaria na Typhod.

Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini


“Baada ya kurudishwa wodini na kulala kwa siku nyingine 3 leo kidogo nimeamka na’vijinguvu’kiasi na ninaweza kuruhusiwa kutoka hospital kurudI nyumbani kumalizia doz zangu za vidonge/sindano kwani pamoja na typhod malaria ilifikia wadudu zaid ya 2000 kiasi ambacho hata madaktari bingwa walishangaa niliwezaje kutembea,kuongea na kuendelea kuwa hai,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Ameongeza, “Ahsanteni sana kwa dua zenu njema amabazo mlikesha mkiniombea na hatimae mwenyezi ameninyanyua tena’undugu si kufanana,undgu ni kusaidiana,kumpa mwenye kuhitaji ni kumkopesha maulana.”

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: