WASANII WA BONGO MUVI WAMLILIA RECHO, WAFANYA MKUTANO KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB LEO JIONI

 Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu
 MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki.
Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders.
 Kwa mujibu  wa mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa ajili ya maziko.  Habari nyingine za msiba zitatolewa wakati wowote na mtandao huu mara tu zinapopatikana.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Steve akizungumza na wanachama wa Bongo Muvi, viwanja vya Leaders.
 Bi. Mwenda akilia kwa uchungu.
 Mume wa Rachel aitwaye Saguda akiwa na majonzi
 Mwigizaji Johari akiwa na huzuni.
 Cathy Rupia  akiomboleza.


Wasanii wa Bongo Muvi wakiwa Muhimbili baada ya kupata habari za kifo cha mwenzao.

PICHA NA GPL

No comments

Powered by Blogger.