JE ELIMU YETU IMEWEZA KUONDOA UJINGA?

Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini matokeo ya sisi ambao tunajiita wasomi au tuliobahatika kwenda shule. Namna tunavyofanya mambo yetu, ukiondoa kuwa na nyumba nzuri, gari, na kazi nzuri. Je Ujinga umeondoka kichwani mwetu? Na tunajuwaje ujinga umeondoka au haukuondoka?
Ujinga wetu tumekuwa wagumu kufanya kitu tunachotakiwa kufanya kama wasomi bali kuendesha mijadala kila siku. Je jamii zetu au familia zetu watajuaje kama ujinga umeondoka? Elimu yetu ilituandaa na inaendelea kutuandaa kwa ajili ya ajira ya kukaa Ofisini. Sababu hii haina tofauti na elimu ya mkoloni, bali vijana na kizazi hiki tunachukua hatua gani kubadilika kulingana na mazingira tuliyonayo?
Tunahitaji kufunguka uelewa wetu na kufanya mambo sahihi, kuzungumza mambo sahihi na kutekeleza vitu sahihi. Tuko kwenye ulimwengu ambao una kila kitu kuliko wale watu wa zamani au zama za Nyerere ila hofu yangu ni kwamba wajinga wanaongezeka ingawa elimu imetawala kila kona na watu wengi wakitumia mtandao.
Ukiingia kwenye mtandao unaweza kujifunza vitu vingi na kwa ukubwa wake, ila tumekuwa tukilalamika kila siku. Wasomi ndio tunaongoza kwa kulalamika na kuandamana halafu watu ambao hawajaenda shule kivile wanafanya kazi na wanajua kufanya kitu sahihi. Je nani ni mjinga? 

 ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

Tuna vijana wetu ambao wanasubiri serikali iwape kazi baada ya kumaliza chuo, hebu fikiri kwamba kazi zinaongezeka kwa kiasi gani na wanafunzi wanaohitimu ni kiasi gani kila mwaka? Inabidi tuache ujinga na tufikiri zaidi, serikali haitatoa ajira kwa watu au vijana wote wanaomaliza kwenye vyuo vyetu tunahitaji kutengeneza ajira kuanzia tukiwa chuoni.
Ukiwa chuoni acha ulimbukeni, fikiria miaka mitatu baadaye utakuwa wapi na unataka kufanya nini? Anza kufikiria na kuwekeza kibiashara na miradi kidogo kidogo mpaka unamaliza chuo kama uko makini utafika mbali. Ukitegemea ajira, habari mbaya ni kwamba sio wote mtakaopata kazi. Hakuna atakayechukulia maisha yako kwa ukaribu ikiwa wewe mwenyewe ni mjinga na haufikirii unakwenda wapi.
Tunakokwenda kunahitaji watu wanaojitambua na wenye uwezo wa kufanya kitu sahihi na kwa umakini.

NA BONGO 5

No comments

Powered by Blogger.