HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» »Unlabelled » PENZI LA SHEMEJI SEHEMU YA AROBAINI NA TISA (49)

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 



 Ilipoishia......
 Wakati najalibu kwa mbinu zangu zote kumshawishi Joan awe mpenzi wangu tulisikia mlango ukigongwa! 

Endelea....... 
Tuligeuka na kuangaliana kwa mshangao sana " Nani anagonga?" tukajikuta wote tukisema neno moja Kisha tukatabasam! Akili kwangu nilijua iwe isiwe huyo ni Shemeji " Nitafanyaje sasa akiwa shemeji?" nikajikuta nikiongea kwa sauti bila kujielewa " Jun jifanye kama unaumwa tafadhali kisha lala mimi ntajua namna ya kufanya" akasema Joan " Akiniuliza kwa nini sijamwambia?" nikauliza " Utamwambia umeona ukimwambia hatafanya kazi vizur na kufunga biashara jambo ambalo sio zuri kibiashara" akajibu 
Nilishangaa kuona yule binti ana mbinu zaidi yangu kwenye sakata kama lile ila hilo likaniaminisha kuwa atakubali kuwa wangu Niliondoka na kwenda chumbani kisha nikafunga mlango kwa funguo na kulala Joan alienda mpaka mlangoni akafungua na kweli akakuta wanaume wawili na mwanamke mmoja " Habari zenu?" aliwasalimia " Nzuri za hapa?" wakauliza " Nzuri,kalibuni" akasema " Tuna shida na wenye nyumba sijui tunaweza kuonana nao?" wakasema " Yupo shemeji peke yake dada yuko kazin" akajibu " 
Hata yeye sio vibaya tukionana naye tafadhali" wakasema " Sawa ingien bas" akawajibu na kuwapisha wapite Baada ya kuwakalibisha sebuleni alikuja kugonga mlango wa chumbani Nilishtuka kusikia mlango ukigongwa na moja kwa moja nikajua ni Shemeji ndiyo amerudi " Shemeji fungua basi" nikasikia sauti ya Joan Nikaamka na kufungua mlango ule kisha nikashangaa akipita moja kwa moja mpaka ndani " 

We kuna nini?" nikauliza " Kuna wageni wanaume wawili na mwanamke mmoja" akajibu Nikashusha presure na kupumua kwa nguvu ila pia nikaona hii ndo nafasi ya kujalibu kuona kama Joan kanikubalia Nikamshika na kumvutoa kwangu kwa nguvu na kisha nikamlazimisha kumla denda Alionesha upinzani kama kitendo kile hakukitaka ila kwa speed na nguvu niliyotumia alijikuta ameshakutana nacho " Kwa nini unanifanyia hivi shemeji? Kwani sisi ni wapenzi? Sio vizur" akasema kwa hasira " 
Am sor bas" nikasema kisha nikamshika kiuno Nilimuona akisisimka na kuruka kwa nyuma kisha akapumua kwa nguvu na kuniangalia kwa aibu " Nenda bana huwezi jua wanakuitia nini?" akasema " Poa" nikajibu Nilijiweka sawa kisha nikaondoka na kuelekea sebuleni na kuwakuta wale watu wamekaa kwenye sofa ya pamoja " Habari zenu jaman? Kalibuni" nikawaambia " Ahsante ndg" wakajibu " 
Ok,sijui niwasaidie nini wapendwa" nikawaambia " Aaah! Wewe ni nani kwenye nyumba hii kijana?" wakauliza " Mimi ndiye mwenye nyumba jaman sasa sijui mnashida gan?" nikasema kwa kujiamin hasa nikijua kuwa baada ya kaka kufa na mimi kumrithi shemeji ndiye mmiliki " Ok,ila tunamjua marehemu Michael kama mmiliki na kwa sababu kafariki tunaamini mkewe ndiye mmiliki sasa sijui wewe ni nan?" waksema " 
Mimi ni mdogo wake na marehemu" nikawajibu " Ok,tufupishe,tunaomba kuonana na shemeji yako tafadhali" wakasema " Yuko kazini kwa sasa" nikawajibu huku nikijiuliza hawa watakuwa akina nani? " Hili swala ni la dharula sana unaonaje ukitupeleka kijana?" wakasema " Kwa nini msije jion akiwa karudi? Kwa sababu kwa sasa mimi nimepumzika" nikajibu 
Nilijibu hivyo kwa sababu kubwa moja,waondoke ili nibaki na kujalibu kupigania penzi la Joan ambalo nilishaona dalili za kulichukua " Hapana kaka tunakuomba sana ni swala la biashara kubwa sana ya faida tunaomba tafadhali" wakasema Nikajikuta nashawishika hasa baada ya kusikia ni biashara kubwa Tukaanza safari kutoka nyumbani bila hata ya kumuaga Joan nikilenga kuwa nitarudi mpaka dukani kwa shemeji 
Kosa moja shemeji alilofanya nilipofika ni kunikumbatia mbele ya hawa jamaa " Ina maana wana uhusiano wa kimapenzi? Lazima kuna namna hapa" walisemezana na tukasikia " Samahani kwa usumbufu jamani,sisi ni maafsa wa polisi kutoka kitengo cha upelelezi,na tumekuja kuwachukua kwa sababu za kifo cha Dokta Rweyemamu" wakasema Nilitoa macho balaa!?!!

ITAENDELEA IJUMAA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: