HABARI

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

MATUKIO

MICHEZO

SIASA

» » » » Lissu asomewa mashtaka ya uchochezi

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi.
Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri leo Jumatatu, Julai 24, mahakama imeelezwa kuwa Lissu ametoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali Julai 17 akiwa maeneo ya Ufipa, Kinondoni.
Imedaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo ya kuleta chuki dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alipotakiwa kukubali ama kukataa makosa hayo na Hakimu Mashauri, Lissu amesema kusema kweli haijawahi kuwa kosa la jinai.
Kwa sasa upande wa mashtaka wameomba Lissu anyimwe dhamana na upande wa utetezi wanapinga hoja ambazo bado zinaendelea.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments: