Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi
Leo usiku wa saa saba kuamkia tarehe 11 June 2017 imetoka taarifa kutoka IKULU Dar es salaam ikiwa na taarifa ya maamuzi mapya ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Leo usiku wa saa saba kuamkia tarehe 11 June 2017 imetoka taarifa kutoka IKULU Dar es salaam ikiwa na taarifa ya maamuzi mapya ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba Waziri Mkuu Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi kuanzia leo tarehe 11 Juni, 2017.
Maamuzi haya yamekuja siku mbili baada ya habari za kampuni ya IPTL kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme ambapo pia Kituo cha sheria na haki za Binadamu kilijitokeza na kusema hakikubaliani na mkataba huo kuongezwa kwani kampuni hiyo inahusishwa na kashfa ya uchotwaji wa Mabilioni kupitia account ya ESCROW.
Hata hivyo baada ya kituo hicho cha LHRC kujitokeza kuongea, EWURA walijitokeza na kusema ‘kuna vitu viwili vya kuzingatia hapa, EWURA tunachodili nacho sasa hivi ni leseni ya IPTL ambayo aliipata 1996 ikiwa ni ya miaka 21 na inaisha July 2017“
No comments:
Post a Comment