TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI: LEO NILIPOKWENDA KUMJULIA HALI MTOTO OMBENI MBEULA ALIYEUNGUA NA MOTO HUU NI MWENDELEZO WA HABARI YA JANA


Mtoto Ombeni anakula mwenyewe leo
 
Leo nilienda kumjulia hali mtoto Ombeni Mbeula ambaye alipata ajari ya moto huko Mpwapwa. Kikubwa zaidi nimepata taarifa nyingine kuhusu mtoto Ombeni Mbeula kwamba alifikishwa hospitalini hapo tarehe 14/12/2012 lakini mpaka jana alikuwa bado hajapata matibabu. Mpaka baada ya blog ya PAMOJAPURE kurusha habari kwenye mtandao na pia mabloger wengine walitumiwa habari kupitia kwenye blog ya PAMOJAPURE ili aweze kusaidiwa kwa matibabu ndipo madaktari wameanza kumpa tiba mtoto huyo.
Kiukweli inasikitisha sana kwa Madaktari wa HOSPITALI YA GENERAL iliyoko mjini Dodoma kutomtibu mtoto Ombeni Mbeula kwa takribani miezi miwili kwa ukosefu wa pesa kutoka kwa familia yake. Isitoshe mtoto  mwenyewe ana miaka mitano (5) inabidi kiutaratibu apate matibabu bure, hivi kweli uongozi wa hospitali ya General umelisimamiaje jambo hili?. Kiukweli inasikitisha kwa madaktari kutomjali mtoto Ombeni Mbeula mpaka habari iliporushwa kwenye mtandao kupitia BLOG YA PAMOJAPURE na washiriki wake wa blog nyingine ndipo madaktari walipoanza  kuitwa lakini hawajaenda kumtibu mtoto huyo.

 Mmiliki wa blog ya PAMOJAPURE akiwa hospitalini kumjulia hali ya mtoto Ombeni

 Hapa mtoto akiwa anaendelea kula chakula mwenyewe
 Mmiliki wa blog ya PAMOJAPURE akiwa hospitalini kumjulia hali ya mtoto Ombeni hapa alikuwa anamweka mtoto huyo vizuri.
 Huyo ndiye mdau mkubwa wa blog ya PAMOJAPURE tulipomtembelea mtoto Ombeni hospitali ya General iliyopo Dodoma Mjini
 ..................................
Kwa moyo wa dhati tunawashukuru wale wote waliotoa michango yao kupitia kupitia kwenye namba ya ndugu yake ambayo ni Ekiria Paskali na namba yake ya simu ni 0757 498336
 
Hawa ni baadhi ya wale walioguswa na tukio hilo na kutoa mchango wao wa hali na mali
jumla ya michango ni shilingi 421,300 mpaka naondoka hospitalini hapo kuna watu walikuwa bado wanaendelea kuchangia. Kama ulikuwa unataka kumchangia mtoto huyu apate matibabu tuma mchango wako kwa kutumia namba hii 0757 498336 mwenye jina lake ni Ekiria Paskali


PICHA KWA HISANI YA PAMOJAPURE BLOG

1 comment

Subi Nukta said...

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na neema akubariki Pamoja Pure blog team kwa wema mnaomfanyia malaika huyu na wengine wengi. Maisha yenu yaone heri na yajae fanaka!

Ombeni, Mwenyezi Mungu akujaalie afya njema na heri katika maisha yako.

Wazazi na walezi, matabibu, wauguzi, waliochangia kwa namna yoyote ile kwa matibabu ya Ombeni, wapate rehema kwa kila jema walilotenda.

Powered by Blogger.