Itikadi za dini, siasa zatawala uchaguzi wa mabaraza

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kushoto) akiwa na Katibu wa Tume Assaa Rashid wakati wa kutangaza tarehe za uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba hivi karibuni.   

Uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba katika ngazi ya serikali za mitaa umnekamilika, kinachosubiriwa ni mikutano ya kata kuteaua wawakilishi wa wane watakaoingia kwenye mabaraza ya wilaya.
Kwa mujibu wa mwongozo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wenyeviti wote na maofisa watendaji wa vijiji na mitaa walishiriki kusimamia chaguzi hiyo na kuwaelekeza wananchi.
Hata hivyo, uchaguzi huo katika maeneo mbalimbali ulitawaliwa na mgawanyiko kwa itikadi za kisiasa na kidini, ambako wananchi walichaguana kwa kuangalia dini na vyama vyao.

Udini katika uchaguzi
Diwani wa Kata ya Kamachumu, mkoani Kegera, Dunstan Mutagahywa (CCM) ni miongoni mwa viongozi walioelezea tatizo hili baada ya kutembelea wilaya za Biharamulo, Muleba, Misenyi, Karagwe na Bukoba Vijiji.
“Nimegundua kuwa kampeni ya udini ilitawala sana na kimsingi maeneo niliyozungukia nilibaini jinsi makundi mbalimbali ya kidini yalivyokuwa yamejipanga kuwapigia kura waumini wao,” anasema.
Anasema jambo hilo limemfanya awe na wasi wasi wa hali itakavyokuwa mwaka kesho na katika uchaguzi ujao, iwapo hali hiyo isiporekebishwa.
“Uchaguzi Mkuu ujao hautakuwa kati ya CCM na vyama vya upinzani, bali utakuwa kati ya ushindani wa wagombea wa dini moja dhidi ya wale wa dini nyingine! Najiuliza tunakwenda wapi?” anahoji katika ujumbe alioutuma kwa gazeti hili.

Mwenendo wa uchaguzi
Kabla ya kuanza kwa chaguzi hizo katika maeneo mbalimbali, viongozi hao waliweka taratibu za watu kujiandikisha, katika karatasi za mahudhurio na baadaye kuhakiki majina ya waliohudhuria, kisha wananchi hao waliwapigia kura ya siri wagombea hao.
Hata hivyo mahudhurio hayakuwa makubwa wala uchaguzi wenyewe haukuwa na hamasa, mathalan, katika Kata ya Kipawa yenye wakazi 60,000 waliojitokeza kupiga kura walikuwa 1,181 na jumla ya wagombea walikuwa 148.

Maoni ya wananchi
Omari Aly Dodo mkazi wa Kipawa, Dar es Salaam anasema uchaguzi haukupangiliwa vizuri lakini wapiga kura walikuwa waelewa na kwa jitihada za oaofisa watendaji walifanikisha uchaguzi huo.
‘’Uchaguzi sio kitu cha kubahatisha, na hili Tume imeonyesha kufanya mambo kwa kubahatisha na bila kujipanga maana hawakutoa karatasi za kupiga kura wala maelekezo ya kina juu ya uchaguzi huu. Ndani ya kata mmoja uendesha wa uchaguzi umetofautiana, hali hiyo sio picha nzuri,” anasema Dodo.
Mkazi mwingine wa kata hiyo, Rutashobya Rutasobya anasema ingawa uchaguzi umekuwa huru na haki lakini hakukuwa na utaratibu mzuri wa kufanisha uchaguzi huo.
Naye Fredrick Kabati kutoka mtaa wa Karakata anasema kumwanchia ofisa mtendaji wa mtaa na mwenyekiti pekee kusimamia wananchi karibia 386 haikuwa sawa.
Katika suala la utaratibu, Kabati anasema pia siku yenyewe ya uchaguzi haikuwa sahihi maana ilikuwa ni siku ya kazi, ambayo imesababisha watu wengi kutohudhuria.
Mkazi mwingine wa kata hiyo, Simoni Makabwa, anasema uchaguzi umefanyika huru na haki ukiachilia changamoto kadhaa zilizojitokeza, lakini anawapongeza wenyeviti wa mitaa na maofisa watendaji wa mitaa kwa kutumia jitihada zao kufanikisha uchaguzi.
Makabwa anatoa angalizo wakati kuchuja majina hayo nakubakiza majina manane ya mtaa, basi kuwepo na maslahi ya Taifa kwanza ili wapatikane watu sahihi.
’Maana hatuja ambiwa watu hao nane wa kata watapatikana kwa sifa zipi basi tunaomba hao wajumbe waongozwe na uzalendo kwa ajili ya nchi yetu,” anasema Makwaba.
Rukia Chacha, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mogo anawashukuru wananchi wa Mtaa wa huo kwa “kujitokeza kwa wingi na kufanikisha tukio hilo” lakini akasema wamekumbana  na changamoto nyingi.
“Hakukuwa na maandalizi, pili vifaa vya uchaguzi kwa maana ya makaratasi na hata masanduku na sehemu ya kupigia kura ilikuwa changamoto,” anasema Chacha.
Mtendaji wa Mtaa wa Karakata Cecilia Chausi anasema uchaguzi umeenda salama, ingawa kulikuwa na mabishano ya hapa na pale, changamoto kubwa imekuwa katika vifaa vya uchaguzi, ambapo walilazimika kutumia fedha zao kufanukisha jukumu hilo.
Kwa upande wake Latifa Mlawa, ofisa mtendaji wa mtaa wa Kipunguni anasema ingawa uchaguzi ulifanyika salama katika mtaa wake lakini changamoto kubwa ilikuwa maandalizi yake duni.
“Tume ya Mabadiliko ya Katiba haikuwashirikisha wadau wa uchaguzi huo, hasa maofisa watendaji wa mtaa na wenyeviti wa mitaa ndio maana changamoto zilikuwa nyingi na tumeendesha chaguzi hizi kwa busara yetu,” anasema Mlawa.
Wananchi mbalimbali waliohojiwa wanansema ili uchaguzi uonekane ni mzuri Tume ilikuwa na wajibu wa kuweka utaratibu mmoja wa jinsi ya kuwachagua wajumbe hao.
Wanasema pia Tume ilitakiwa kuweka muda mmoja na siku moja kwenye kata nzima ilikuwadhibiti wapiga kura kushiriki zaidi ya sehemu moja.
Kuhusu mahudhurio hafifu, wananchi hao wanasema uhamasishaji ulikuwa mdogo na siku ya kazi.

Nachingwea na itikadi za vyama
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rajabu Macholilo anasema uchaguzi umefanyika salama ingawa kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwamo wananchi kuchaguana kwa kuangalia vyama badala ya maslahi ya Taifa kwanza.
Kata yake inajumuisha vijiji vitatu vya Kilimahewa, Nachingwea na Dodoma.
Akifafanua anasema kulikuwa na changamoto ya mahudhurio na cha ajabu  katika Kijiji cha Kilimahewa hakuna mwanamke hata mmoja aliyejitokeza kugombea.
Anasema katika Kijiji cha Nachingwe wanawake walijitokeza lakini hawakupata kura hata moja.



MWANANCHI

No comments

Powered by Blogger.