LEMA AFANYA MAANDAMANO MAKUBWA BAADA YA KUPEWA DHAMANA LEO ASUBUHI

 Asubuhi ya leo, kama ilivyotarajiwa na wengi baada kufuatia taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa Arusha baada ya kukaa rumande tangu alipokamatwa usiku wa kumkia siku ya Jumamosi, Aprili 27, 2013.

Mbele ya hakimu Devotha Msofe na mawakili Kimomogoro na Humphrey Mtui wanaomtetea, Lema amesomewa shitaka la kosa la uchochezi linalomkabili kwamba aliwachochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha kumzomea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kuwaambia wanafunzi kuwa Mkuu huyo wa Mkoa, “hajui chuo cha uhasibu kilipo, amekuja akiwa amechelewa na anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.”

Hata hivyo, mtuhumiwa Lema amekana kosa hilo. Mwendesha mashitaka alisema dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa endapo atatimiza masharti ya dhamana. Mtuhumiwa alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwepo kwa mtu mmoja mwenye kitambulisho kinachokubalika kisheria na kuweka rehani kiasi cha shilingi milioni moja. Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 29 Mei mwaka huu. Source: http://www.wavuti.com
 

 Wanachama wa CHADEMA wakishauriana baada ya kuambiwa walipe shilingi milioni moja kwa ajiri ya dhamana yake
 Ili ni mojawapo la mabango yaliyokuwa yamebebwa na raia mahakamani leo asubuhi
 Maandamano yalianza rasmi kutoka mahakamani

 Lema na Nasari wakiwa wamepanda juu ya gari wakiwapungia wananchi mikono

 
 Baada ya kutoka mahakamani hapo, Lema alielekea kwenye maeneo ya Ofisi za chama, CHADEMA.
Ili ni mojawapo la mabango yaliyokuwa yamebebwa na raia mahakamani leo asubuhi

No comments

Powered by Blogger.