YALIYOJIRI KWENYE MAADHIMISHO YA 19 YA MAUAJI YA KIMBARI YALIYOTOKEA NCHINI RWANDA YALIYOFANYIKA JIJINI DAR JANA
Maandamano ya raia wa Rwanda wanaoishi nchini Tanzania pamoja na
wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakijipanga katika
ukumbi wa New World Cinema tayari kuanza maandamano ya kuadhimisha
miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda kuelekea ukumbi wa mikutano wa
Mlimani City. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Picha juu na chini Umati wa maandamano yakielekea katika ukumbi huo.
Mgeni
rasmi Dr. Salim Ahmed Salim (wa tatu kulia) akiwa na balozi wa Rwanda
nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi (wa tatu kushoto) wakisubiri
kupokea maandamo ya maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari ya
Rwanda katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar.
Dr. Salim Ahmed Salim akipokea rasmi maandamano hayo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho ya 19 ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda Dr. Salim
Ahmed Salim akizungumzia kumbukumbu ya mauaji hayo ambapo amesema
historia ipo kwa ajili yetu sote kujikumbusha yaliyopita ili tuweze
kupanga yajayo na kuwa mauaji ya Kimbari ni mzigo wetu sote na tunapaswa
kujifunza kutambua alama za watu wa jamii moja kuanza kuhitilafiana na
kutafuta namna ya kuzitatua kabla hazijaleta athari.
Na
pia alichukua fursa hiyo na kunukuu maneno yaliyowahi kusemwa na Baba
wa Taifa wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere " Ukweli ni
kwamba kila sehemu ya Afrika ina ihitaji Afrika kwa pamoja na Afrika
kama bara inahitaji kila sehemu ya bara la Afrika".
MC katika maadhimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Usia Nkhoma
akirekebisha kipaza sauti wakati mgeni rasmi akizungumza wakati wa
maashimisho hayo.
Wageni
waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa
kumbukumbu ya maashimisho ya miaka 19 ya mauaji ya Kimbari Rwanda.
Kaimu
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Jama Gulaid ambaye pia ni
Mkurugenzi Mkazi wa UNICEF akizungumza wakati maadhimisho ya miaka 19 ya
mauaji ya Kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo
katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo amesema dunia nzima
itakuwa na siku maalum ya kukumbuka wahanga wa mauaji ya Kimbari ya
Rwanda kwa heshima ambayo ni alama ya kukumbuka athari za mauaji hayo na
kuwa pamoja na walionusurika na kwa namna nyingine ni alama msingi ya
kupongeza hatua zilizochukuliwa na jamii ya Wanarwanda kuungana pamoja.
Katika
mazungumzo yake alinukuu maneno yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Ban Ki Moon " Katika maasdhimisho ya 19 ya mauaji ya Rwanda
tunawakumbuka watu zaidi ya 800,000 wasio na hatia ambao walipoteza
maisha yao na tutanendelea kuwaheshimu walionusurika na tutaendelea kuwa
nao pamoja na kukemea wale wote waliohusika na tukio hilo, na
kuwapongeza waliojitokeza kuzuia mauaji hayo yasiendelee".
Balozi
wa Rwanda nchini Tanzania Mh. Benjamin Ruganganzi akitoa salamu zake
kwa wageni waalikwa pamoja na watu waliohudhuria maadhimisho ya 19 ya
mauaji ya Kimbari ya Rwanda na kuhakikisha kuwa wananchi wa Rwanda
wataendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano pamoja na nchini zingine
za Afrika Mashariki ili kuhakikisha tukio kama hilo halitajirudia tena.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo mabalozi mbalimbali wakimsikiliza Balozi wa Rwanda nchini (hayupo pichani).
Msemaji
wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda (ICTR) Bw. Roland
Ammousouga akitoa kauli yake wakati wa maadhimisho ya 19 ya mauaji ya
Kimbari ya Rwanda ambapo amesema kwa miaka 19 iliyopita watu wanaweza
wakajisifu kazi iliyofanywa na mahakama ya ICTR kwamba imetimiza kilio
cha maelefu ya waathirika na kuwa imesaidia katika kuleta upatanishi na
kuijenga upya Rwanda sambamba na kuhamasisha amani na ulinzi katika
ukanda wa Afrika wa maziwa makuu, wakati haikufanikiwa kuwakamata wale
wote waliohusisha na mauaji hayo kwa kutoa itumia Rwanda kuwatafuta
wahusika 6 waiojulikana walipo ili waweze kukabiliana na kesi
zinazowakabili kinachojionyesha hapa ni kwamba ICTR inaashiria kwamba
mapambano dhidi ya mazingira ya wahusika wengine 3 hawawezi kukamatwa.
Umati wa watu waliofurika (chini) katika maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee (juu).
Mmoja wa viongozi wa Dini akiomba dua ya kuwarehemu walipoteza maisha katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Meza
kuu ikiongozwa na mgeni rasmi Dr. Salim Ahmed Salim kuwasha mishumaa
ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mauji
ya Kimbari nchini Rwanda.
Post a Comment