YALIYOJIRI KWENYE TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 NDANI YA UWANJA WA MKWAKWANI MKOANI TANGA


Msanii Neylee akiimba kwa hisia jukwaani.
 Wasanii wa kundi la Wanaume TMK likiongozwa Chege na Themba wakiwaimbisha mashabiki wao jukwaani
 Pichani ni Mwana FA na swahiba wake AY wakilishambulia jukwa kwa pamoja 

 ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria,Jay Martins akiwaimbisha mashabiki wake kwenye tamasha la Serenget fiiesta 2013 ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga usiku wa kuamkia leo,ambapo maelfu ya wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi uwanjani hapo kushuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la tamasha hilo.
Maunda Zorro akiimba jukwaani ndani ya tamasha la serengeti fiesta usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Christina Bella akiwaimbisha mashabiki wake.
Mashabiki wakifuatilia yanayojiri jukwaani usiku wa kuamkia leo.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Tanga waliojitokeza kwa wingi usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa mkwakwani mkoani Tanga
Msanii wa hip hop anaekuja juu katika anga ya muziki huo,Stamina akiimba jukwaani
Pamoja na manyunyu ya mvua kusumbua sumbua hapa uwanjani,lakini mashabiki wala hawakutaka kubanduka uwanjani hapa usiku huu.
MKali kutoka shindano la BSS,Walter Chilambo akiwaimbisha mashabiki wake-
Watu kibao usiku huu.
Pichani kati ni msanii Ally Nipishe akiwa na madansa wake jukwaani
mashabiki kutoka kila kona walikuwepo.
Mashabiki wakishangwekwa vilivyo usiku wa kuamkia leo.
Godzilla akikamua mbele ya mashabiki wake.
Linah akicheza na shabiki wake jukwaani-
Shilole na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja huku miluzi na mayowe ikiwa imetawala kila kona ya uwanja.

Gea Habib na mdau wake wakilifuatilia jukwaa la fiesta vilivyo yaliyokuwa yakijiri.


No comments

Powered by Blogger.