KAMANDA WA POLISI DODOMA AKUTANA NA KUONGEA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA TARAFA YA DODOMA MJINI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akiongea na Viongozi mbalimbali wa Tarafa ya Dodoma Mjini na kutoa maelekezo ya ulinzi na usalama.
Afisa tarafa Dodoma Mjini HEMEDI HUSSEIN na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP wakisoma baadhi ya maelekezo kwa viongozi wa Kata na Vitongoji vya Dodoma mjini alipokutana na viongozo hao. 

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI


Mch. JOSHUA MTAKYAMA wa KKKT Nkuhungu Dodoma akichangia jambo katika kikao hicho.
Viongozi mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Polisi Moa wa Dodoma David Misime - SACP.

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema jukumu la kwanza la serikali za mitaa ni kuwahakikishia wananchi wake usalama, amani, utulivu na utengamano hivyo ni jukumu la watendaji wa kata, mwenyekiti wa Mitaa na vitongoji kusaidia kuimarisha ulinzi katika maeneo yetu.

Amesema hayo alipokutana na Viongozi wa mbalimbali wa Tarafa ya Dodoma mjini katika Ukumbi wa Polisi Dodoma wakiwemo Madiwani, Afisa tarafa, Watendaji wa Kata, Wenyekiti wa Serikali za mitaa, Vitongoji na Viongozi wa Dini na kusisitiza masuala ya ulinzi na usalama katika kipindi hiki cha tukio la kihistoria la kupata Katiba mpya.

Kamanda MISIME ameongeza kuwa kuwaambia wenyekiti wa serikali za mitaa kuvifufua vikundi vya ulinzi shirikishi hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa kupata katiba mpya ili kuweza kuzuia uhalifu hasa wa uvunjaji.

Aidha Kamanda MISIME amewaomba viogozi hao kushirikiana katika kupunguza ajali za usalama barabarani pamoja na kujenga utamaduni wa kusema familia yangu haina uhalifu.

Pia Kamanda MISIME amewataka wamiliki wote wenye baa na Kumbi za starehe kuzingatia sheria za kufungua na kufunga baa na kumbi hizo kwani zimekuwa ni sehemu ya maficho ya wahalifu.

No comments

Powered by Blogger.