JIFUNZE KUONGEZA UWEZO WAKO WA KUONGOZA


1. Wape Changamoto ya unawaongoza kutokubaliana na kila kitu unachosema
Makampuni yanapata shida kwa sababu kila mtu anaogopa kuongea ukweli wa mambo. Mabosi huwa hawapendi kuambiwa ukweli wanataka kuambiwa wanachotaka kukisikia. Kama unataka kuongeza uwezo wako wa kuongoza ruhusu watu unaowaongoza wakuambie ukweli wa kila unachoongea, kama ni kibaya ruhusu waseme. Pindi utakapoaanza kufanya hivyo na uwezo wako wa kuongoza utaanza kubadilika.

2. Wawezeshe walio chini yako
Unapowawezesha walio chini yako, unawafanya waweze kufanya unachofanya. Kwa kufanya hivyo unaongeza uwezo wako wa kuanza kufanya vitu vingine vikubwa zaidi.

3.Wanapokosea, usiwaharibu
Unaowaongoza wape nafasi ya kujifunza kila unachowafundisha, vile vile wajifunze kutokana na makosa wanayofanya na sio kuwafukuza au kuharibu taaluma zao.

4. Onesha Kujali
Onyesha kuwajali unaowaongoza, weka uhusiano wako vizuri kati yako na wao itawafanya wakupende na kupenda kazi kwenye idara yako.

ENDELEA KUSOMA MAKALA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 5. Kusudia kujifunza kila siku
Hebu jiulize, “je ni kitu gani sikijui na ninapaswa kukijua katika taaluma na uongozi wangu? Je ninajifunzaje ?

6. Jitambue
Anza safari ya kujitambua mwenyewe tabia na mwenendo wako halisi katika maisha yako binafsi. Unapoongoza watu usisahau kwamba wewe ni binadamu na kila unachokifanya watu wanakiona hivyo watakuheshimu au kukudharau kulingana na tabia na mwenendo wako binafsi.

7. Zingatia Malengo kwa kusimamia lengo
Unaweza kuwa na malengo mengi kama kiongozi inabidi usimamie lengo moja kubwa na kulifanikisha kwa wakati fulani ndipo uelekee kwenye lengo jingine.

8. Fukuza mameneja wabovu
Katika utendaji wako kama kiongozi hakikisha una timu ya watu ambao wanajifunza na wanafanya kazi vizuri kwa kuonyesha ongezeko na ubora wa kile wanachokifanya. Kama kiongozi, usipuuzie uzembe, uvivu na kurudishwa nyuma na watu ambao hawawajibiki ipasavyo.

9. Tumia ujuzi wa uongozi kila siku
Kila unapotumia ujuzi wa uongozi kila siku, inakusaidia kukuongezea ufanisi na ubora wa uongozi wako. Jifunze nadharia halafu uweke katika matendo, na itakufanya uwe kama unasikiliza mziki mzuri katika utendaji wako.

No comments

Powered by Blogger.