WASIOONA WAOMBA FIMBO NYEUPE

 Mratibu wa Mradi wa Ulingo wa Majadiliano kuhusu ujumuishwaji, Utetezi wa Mahitaji na Haki za Wenye ulemavu wa Macho (Wasioona) Mathias Fwejeje akionyesha Fimbo nyeupe zinazotumiwa na wasiiona, Walemavu hao wa Macho wanahitaji fimbo 110 ili waweze kuepukana na Ajali.
 Mratibu wa ulingo wa majadiliano kuhusu ujumuishwaji wa walemavu wa macho [wasioona] Mathias Fwejeje  katika utetezi wa mahitaji yao na haki katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUOFYA HAPA CHINI


  Diwani wa kata ya Mnadani Stiven Masangia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Ulingo wa Majadiliano kwa walemavu wa macho waliokutana kujadili namana watakavyofikisha kilio chao kwa serekali ili nao washirikishwe katika utetezi wa haki zao katika maamuzi.
Walemavu hao wa Macho wakiwa ukumbini kwa ajili ya majadiliano hayo.

 Na John Banda, Dodoma
CHAMA cha wasioona Tanzania [TLB] manispaa ya Dodoma kinahitaji msaada wa kununuliwa fimbo nyeupe za kuwatambulisha wanapokua barabarani ili kunusuru maisha ya wanachama wao. Hayo yalisemwa na Mratibu wa mradi wa Ulingo wa majadiliano  kuhusu
uwezeshwaji, ujumuishwaji na utetezi wa mahitaji na haki za wenye ulemavu wa macho Mathias Fyejeje waliokutana miyuji Dodoma.
Fyejeje alisema tatizo hilo la ukosefu wa fimbo nyeupe kwa wasioona ni tatizo kutokana na kusababishiwa ajali za mara kwa mara ambapo mpaka sasa tayali wanachama wawili wamegongwa japo hawakuathiliwa sana kiasi cha kuwafanya kushindwa kutembea.
Alisema kazi kubwa ya fimbo hizo nyeupe ni kumtamburisha asiyeoona anapokua barabarani kwa madereva na watembea kwa miguu kwani anakuwa hawezi kukwepa hatari yoyote bali huyo anayeona anapaswa kufanya hivyo kutokana nan a kuiona fimbo hiyo.
Mratibu huyo alisema uhitaji ni fimbo 150 kutokana na idadi ya wasioona waliopo katika chama hicho cha Wilaya ambazo kila moja inauzwa kati ya 30,000 na 35,000 kwa moja na hivi sasa wamekwishapokea fimbo 40 toka kwa wahisani mbalimbali na hivyo kusaliwa na 110 mpaka hivi sasa.
‘’Umuhimu wa fimbo nyeupe ni mkubwa kwa wasioona kwa sababu pamoja na kumuongoza lakini ni kitamburisho njiani ili waenda kwa miguu na madereva waweze kuwajua kuirahisi hali itakayowaepushia ajali za mara kwa mara’’, alisema Fyejeje
Aidha aliongeza kuwa miundo mbinu kwa kwa wasioona ni tatizo hasa kwa majengo na barabara ambapo ameshauri ngazi zote za majengo ziwe na vizuizi vya pembeni, Mifeleji  na madaraja yakewe tahadhari ya watu wenye ulemavu huo ili wasipate tabu wanapoitumia.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mnadani manispaa ya Dodoma Stiven Masangia aliyefungua ulingo huo wa majadiliano aliwataka wahisani mbalimbali mbali kuwanunulia fimbo hizo na serikali kuwajengea miundombinu rafiki ili kuepusha ajali zisizo za lazima kwa wasioona.

No comments

Powered by Blogger.