AJALI YATOKEA JETI LUMO BAADA YA KONTENA LA GARI YA MIZIGO KUANGUKIA GARI YA ABIRIA AINA YA HIACE JIJINI DAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Kumetokea ajali mida hii maeneo ya Jeti Lumo mwisho wa lami ambapo gari kubwa la mizigo limeangua daladala iliyokuwa kituoni.
Ajali hiyo imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa lami ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.
Mtoa taarifa wangu amesema hali ni mbaya na bado hajajua idadi ya vifo na majeruhi ujumla.Pia gari imepondeka sana jambo ambalo linaashiria hatari zaidi.
Kuna gari la kunyanyua makontena limeshafika pale lakini limeshindwa kutoa msaada wa uhakika kutokana na kuzidiwa uzito na kontena ambapo likijaribu kunyanyua kontena ushuka chini na kuzidi kuongeza maafa.

 HABARI NA MDAU WETU GOODLUCK ANDREW

No comments

Powered by Blogger.