KINANA ALAKIWA KWA SHANGWE MTWARA VIJIJINI, ATOA HESHIMA KWENYE MNARA WA SHUJAA HAMAD MZEE ALIYETUNGUA NDEGE MBILI ZA KIRENO KATIKA VITA VYA UKOMBOZI WA MSUMBIJI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.


 Wananachi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili Wilaya ya Mtwara Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 



 Kinana akizungumza wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kibaoni, Mtwara Vijijini leo.


 Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Katika Kijiji cha Nanguruwe, Wilaya Mtwara Vijijini


 Mzee Ismail Lumbeya (95), akisikiliza kwa makini wakati Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Nanguruwe



Mnara wa Kumbukumbu ya Mwanajeshi wa Tanzania , Hamad Mzee aliyeuawa na ndege ya kivita ya wareno baada ya kuzitungua ndege mbili za kivita mwaka  1972 katika Kijiji cha Kitaya mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakati wa mapambano ya kuikomboa Msumbiji


 Kinana akitoa heshima katika mnara wa kumbukumbu shujaa Hamad Mzee katika Kijiji cha Kitaya, Mtwara Vijijini


 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa hadhara katika Kata ya Kitaya


 Ngoma ya asili ikitumbuiza wakati wa mkutano huo


 Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo




Kinana akihutubia katika mkutano huo


 Kinana akipanda katika moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwa makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini katika mkutano wa hadhara wa katika Kata ya Kitaya.

Kinana akimkabidhi kadi ya CCM mmoja wa wanachama wapya wa chama hicho katika mkutano huo

 Watoto wakiwa na vipeperushi vya picha ya Kinana wakati wa mapokezi yake katika Kijiji cha Kibaoni


 Kinana akikunjua bendera wakati wa uzinduzi wa Tawi la CCM la Vijana akatika Kijiji cha Nanyamba


 Kinana akitoka kukagua mradi wa maji katika Kata ya Nanyamba Mtwara Vijijini


 Vijana wakicheza ngoma ya madudu katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Nanyamba



 Kinana akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe kinachotarajiwa kuwa hospitali ya wilaya Mtwara Vijijini


Kinana akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nanguruwe.
PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


No comments

Powered by Blogger.