ATLETICO MADRID YAKUBALI KICHAPO CHA MABAO 3-2 KUTOKA KWA FC BARCELONA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Neymar akiifungia timu yake ya Barcelona bao kwenye Uwanja wa Vicente Calderon na kuitoa timu ya  Atletico Madrid kwenye mashindano kwa mabao 3- 2.
 Barcelona imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme, Hipsania ikijulikana kama Copa del Rey  baada ya kuilaza mabao 3-2 Atletico Madrid, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla 4-2.

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Fernando Torres aliifungia Atletico sekunde ya 39, kabla ya Barcelona kusawazisha dakika ya tisa.
Luis Suarez akamsetia Mbrazil, Neymar kuifungia bao la pili Barca, kabla ya Raul Garcia kuisawazishia Atletico Madrid dakika ya 11.
Miranda akajifunga kuipatia bao Barca bao la tatu, kabla ya Gabi kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kikosi cha Atletico Madrid; Oblak, Juanfran/Gamez, dk58), Gimenez de Vargas, Miranda, Siqueira; Raul Garcia, Gabi, Suárez, Turan/Cani, dk63), Griezmann/Níguez, dk45 na Torres.
Barcelona; Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano/Mathieu dk61, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Neymar/Pedro, 77.(Picha na Yahoo)

No comments

Powered by Blogger.