RAIS KIKWETE AWASILISHA RIPOTI YA KAMATI YA VIONGOZI JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.



Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasilisha ripoti ya utendaji wa kamati hiyo katika mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Addis Ababa Ethiopia.Mkutano huo ulimalizika jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Afrika Juu ya mabadiliko ya Tabia nchi(The Committee of African Heads of State and governments on Climate change) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimakabidhi nakala ya Ripoti ya utendaji mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Rais wa Misri Abdel Fattah el Sisi wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa Ethiopia.Rais Kikwete alipongezwa kwa kuiwezesha kamati hiyo kupata mafanikio makubwa.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Sweden,Stefan Lofven jijini Addis Ababa Ethiopia jana.Tayari Rais Kikwete amerejea nchini baada ya kumaklizika mkutano wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika AU jijini Addis Ababa Ethiopia uliofanyika kwa siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa 23 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ulifanyika katika mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa. (picha na Freddy Maro).

No comments

Powered by Blogger.