Kambi ya Lowassa yateka UVCCM
|
Waziri Mkuu Mstaafu,Mheshimiwa Edward Lowasa
KAMBI ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa imeendelea kuyanyanyasa makundi mengine ndani ya CCM, ambayo yamekuwa yakijipanga kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.Kambi ya kiongozi huyo ni kama imehamia Dodoma ili kuhakikisha watu wake wanashinda katika chaguzi za viongozi wa juu wa jumuiya za CCM baada ya kufanikisha kile inachodai kuwa ushindi mkubwa katika ngazi za wilaya na mkoa kutokana na watu wake wengi kushinda. |
Wapambe wa Lowassa wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter
Serukamba na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), Hussein
Bashe wapo Dodoma kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa
Jumuiya ya Wanawake (UWT) na wataendelea kuwapo mpaka jumuiya zote
zitakapokuwa zimefanya uchaguzi huo.
“Hapa kazi ni moja tu,
hakuna kulala maana tukilala tutajikuta tumewekwa pabaya. Tumefanikiwa
UWT na sasa tunaelekeza majeshi yetu UVCCM... lazima tuhakikishe
tunakomesha uonevu wa kuitana magamba mwaka huu,” alisema mmoja wa
wapambe wa Lowassa juzi usiku.
Matokeo ya uongozi wa juu wa UWT
yameongeza matumaini kwa kambi hiyo ambayo imezoa zaidi ya asilimia 80
ya viongozi katika jumuiya hiyo yenye ushawishi mkubwa katika uamuzi
mbalimbali wa chama hicho.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba
ambaye alitetea vizuri nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame
wanatajwa kuwa katika kambi hiyo huku wajumbe saba kati ya tisa
waliochaguliwa kuiwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa
(Nec) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambo hiyo.
Walioshinda
nafasi za ujumbe wa NEC ambao wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa ni
pamoja na Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa, Waziri wa zamani wa
Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana.
Wengine ni wabunge wa Viti Maalumu, Diana Chilolo, Zainabu Kawawa, Mary Mwanjelwa na Subira Mgalu.
Wajumbe wawili ambao ni pamoja na Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene yeye anatajwa kuwa hana kundi lolote wakati Mbunge wa Viti Maalumu, Betty Machangu ambaye anatajwa kwamba alikuwa akimuunga mkono Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela.

Kilango ambaye alikuwa akiungwa
mkono na makundi ya watu waliojipambanua kuwa wapambanaji na ufisadi,
aliangushwa vibaya na Simba kwa zaidi ya kura 400 katika kinyang’anyiro
cha nafasi ya Mwenyekiti wa UWT.
Vigogo wengine wanaotajwa kuwa na kambi katika kinyang’anyiro hicho cha urais wa 2015 ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambao katika uchaguzi wa jumuiya za CCM nguvu zao zinaonekana kuwa si kubwa kama ilivyotarajiwa.
JK awapasha viongozi UWT
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete juzi usiku aliwatolea uvivu viongozi wa UWT, akiwataka kuchukua hatua za kumaliza nyufa zilizosababishwa na uchaguzi uliomalizika Jumamosi iliyopita.

Rais Kikwete alisema
viongozi waliochaguliwa wakiongozwa na Simba ambaye pia Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wachukue hatua kuondoa makundi
ambayo yanatokana na uchaguzi.
“Hii jumuiya siyo yenu, ni ya
wanachama kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima muwe tayari kufanya kazi na
kila mmoja, isije ikawa ni wale marafiki zako tu maana ikiwa hivyo
utamteua hata kama uwezo hana,” alisema Kikwete alipokuwa akifunga
mkutano huo wa uchaguzi mjini Dodoma.
Alikemea tabia ya chuki
inayojengwa na uchaguzi akisema inatokana na viongozi walioko katika
nafasi mbalimbali za uongozi kudhani kwamba wanazimiliki binafsi.
“Hupaswi
kumchukia mtu eti kwa sababu amegombea nafasi fulani, hakuna nafasi ya
mtu, nafasi zote ni za chama, kwa hiyo kama ulikuwa mwenyekiti, uongozi
wako unakoma pale tunapotangaza upya uchaguzi,” alisema Rais Kikwete na
kuongeza:
“Tukishatangaza kila mwanachama mwenye sifa anakuwa na
haki ya kugombea nafasi hizo, sasa wewe usimchukie na kumuuliza eti kwa
nini unagombea nafasi yangu, siyo nafasi yako, hii ni nafasi ya chama.”
Alikemea tabia ya baadhi ya viongozi au wagombea kuwajengea chuki wale ambao hawakuwaunga mkono, na kwamba anayefanya hivyo hapaswi kuwa kiongozi.
Alikemea tabia ya baadhi ya viongozi au wagombea kuwajengea chuki wale ambao hawakuwaunga mkono, na kwamba anayefanya hivyo hapaswi kuwa kiongozi.
Alisema
kiongozi wa aina hiyo daima ataongoza kwa makundi, akiwapenda wale
waliomuunga mkono na kuwatenga wale ambao walikuwa na mtazamo tofauti
jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa jumuiya na chama kwa jumla.
“Kila
mwanachama ana uhuru wa kumuunga mkono mtu anayempenda, sasa wewe
unapomkasirikia na kumjengea chuki unamaanisha nini? Demokrasia maana
yake ni kila mmoja wetu kumchagua mtu anayeona anafaa,” alisema.
Alitoa
mfano kwamba baada ya yeye kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia CCM
mwaka 2005 na baada ya uchaguzi uliompa ushindi, aliwateua wale
waliokuwa washindani wake katika Baraza la Mawaziri, akiwamo Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya.
“Mwandosya
tuko naye hadi leo, hata wale waliokuwa wakinipinga na wengine
walinifanyia mambo ya ajabu kwelikweli, lakini hayo yote inafika mahali
unaweka kando maana huwezi kuongoza nchi kwa kuwateua marafiki zako tu,”
alisema Kikwete.
Uchaguzi UVCCM leo
Rais Kikwete leo anatarajia kufungua Mkutano wa Nane wa UVCCM utakaofanyika katika Chuo cha Mipango, Dodoma huku vita kubwa ikitarajiwa katika uchaguzi kwa misingi ya kambi za urais kuelekea 2015.
Vita kubwa katika uchaguzi huo ni katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo inawaniwa na Paul Makonda, Mboni Mhina na Ally Salum Hapi, wakati nafasi ya Mwenyekiti inawaniwa na Sadifa Juma Khamis, Rashid Simai Msaraka na Lulu Msham Abdallah.

Katika nafasi ya umakamu, Makonda anaungwa mkono na
kambi ya Membe, wakati kambi ya Lowassa imeamua kuelekeza nguvu zake kwa
mwanadada, Mboni. Kambi hiyo pia inamuunga mkono Sadifa anayegombea
nafasi ya Uenyekiti.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema
jumuiya yake inafuatilia mienendo ya wagombea wote na wapambe wao na
kwamba watakaobainika kukiuka taratibu za uchaguzi watachukuliwa hatua.
Akizungumzia suala la rushwa ambalo linaonekana kuiandama CCM pamoja na jumuiya zake, Shigela alisema: “Katika hilo tumejipanga vizuri kukabiliana nalo.”
Akizungumzia suala la rushwa ambalo linaonekana kuiandama CCM pamoja na jumuiya zake, Shigela alisema: “Katika hilo tumejipanga vizuri kukabiliana nalo.”
“Mfano mzuri ni kule Zanzibar, katika Mkoa wa Mjini
Magharibi tumetengua nafasi za wajumbe wawili wa Baraza, hii ni
kuonyesha kuwa hatutanii lazima watu wawe waadilifu,” alisema.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya Umoja wa Vijana, mkutano huo utakuwa chini ya
Uenyekiti wa Benno Malisa kwani kanuni inasema kama mwenyekiti si
mgombea, basi ndiye atakayeongoza mkutano huo.
Mkutano huo pamoja na kuchagua viongozi wa UVCCM, pia utapitisha katiba mpya ya jumuiya hiyo.
Mkutano huo pamoja na kuchagua viongozi wa UVCCM, pia utapitisha katiba mpya ya jumuiya hiyo.
Post a Comment