BENKI YA CRDB YAKABIDHI JENGO LA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO
Jengo
la Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ikionekana ikiwa
katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya CRDB na
kugharimu kiasi cha sh. milioni 50.(Picha na Father Kidevu)
Meya
wa Manispaa ya Morogoro Amir Nondo (kushoto) akifurahjia jambo na
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa (kati)
na Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey.
Wafanyakazi
wa benki ya CRDB wakiwa wameshika miche ya miti tayari kwa kuanza zoezi
la upandaji miti kuzunguka katika maeneo ya hospitali ya Mkoa wa
Morogoro.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akipanda mti wa kumbukumbu
baada ya uongozi wa benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika
hospitali ya Mkoa wa Morogoro lililofanyiwa ukarabati pamoja na kuwekewa vifaa
muhimu katika wodi hiyo. Jumla ya Sh. Milioni 50 zimetumika katika ukarabati
huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akipanda
mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya kukabidhi wodi ya watoto katika hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati), akishiriki kufanya usafi katika
jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambayo imefanyiwa
ukarabati mkubwa na benki ya CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo
Dk. Charles Kimei akishiriki katika zoezi la kufanya usafi. Hafla hiyo
ilifanyika mjini Morogoro juzi. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir
Nondo.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (katikati) akipokea mfano wa ufunguo kutoka
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakati wa kukabidhi
jengo la wodi ya watoto ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ambayo
imefanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo. Hafla hiyo imefanyika mjini Morogoro
juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa benki ya CRDB tawi la Morogoro, Pendo Assey.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizindua wodi ya watoto katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Kutembelea wodi ya watoto.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akitandika kitanda baada ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi jengo la
wodi ya watoto lililofanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitandika kitanda baada
ya uongozi wa Benki ya CRDB kukabidhi jengo la wodi ya watoto
lililofanyiwa ukarabati mkubwa na benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kufanyiwa ukarabati na Benki ya
CRDB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Charles Kimei.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (kulia), na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei wakiweka
chandarua katika kitanda wakati walipotembelea wodi ya watoto katika
hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya uongozi wa benki ya CRDB
kukabidhi jengo la wodi hiyo ambayo imefanyiwa ukarabati mkubwa na
benki hiyo. Kulia aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Juma
Ngasongwa.
Picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB
Dk. Charles Kimei akiingia ukumbini wakati wa hafla iliyoandaliwa na
benki hiyo kwa ajili ya wateja wao.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma
kwa Wateja, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa na
benki hiyo kwa ajili ya wadau wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Dk.
Charles Kimei akizungumza na wadau wa benki hiyo katika ukumbi wa
Nashera mjini Morogoro.
Msanii Mrisho Mpoto wa Mjomba Band akiimba kwa hisia. Kulia ni mwimbaji wa benki hiyo, Ismail Kipira.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Juma Ngasongwa ambaye kwa sasa ni mkulima wa Mpunga akiwa na wadau kataika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akikata keki na Mkurugenzi wa tawi la Morogoro, Pendo Assey.
Mdau wa benki ya CRDB, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo akipata keki.
Wateja mbalimbali wakipa keki.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kushoto) akiwa na maofisa wa benki hiyo.
Post a Comment