MELI YA KOREA KUSINI YAZAMA, ABIRIA 293 HAWAJAPATIKANA

Meli ya Korea Kusini ikizama.
  Meli hiyo ilikuwa na watu 459 kati ya hao wanafunzi waliokuwa wamepanda meli hiyo walikuwa ni 325 ambayo ni asilimia 95 ya abilia waliokuwa wamepanda meli hiyo wakielekea kwenye utarii katika kisiwa cha Jeju
Watu walionusurika wamekuwa wakielezea hali ilivyokuwa ya kutisha ndani ya meli ya Korea Kusini ilipoanza kusimama kwa kuyumba, akiegemea upande mmoja na haraka kuanza kuzama.
"Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikanza kuegemea upande mmoja," amesema abiria aliyeokolewa, Kim Song-Muk.

ENDELEA KUTIZAMA TUKIO HILI KWA KUBOFYA HAPA CHINI


"watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka."
Bado haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa iliwabeba wanafunzi wa shule, lakini watu walionusurika katika ajali hiyo wanatoa maelezo sawa kuhusu tukio hilo la kutisha.
Kikosi cha Walinzi wa Pwani ya Korea Kusini kimesema abiria wapatao mia tatu hawajulikani walipo baada ya meli kupinduka na kuzama.
 
Inasemekana watu mia moja na sitini na wanne wameokolewa. Kikosi cha wapiga mbizi kwa sasa wanatafuta meli iliyozama. Wengi wa abiria wa meli hiyo ni wanafunzi wa sekondari wakiwa katika safari ya masomo kuelekea kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.

CHANZO: YAHOO

No comments

Powered by Blogger.