SIKILIZA NA DOWNLOAD NYIMBO YA TANZANIA TUULINDE (MUUNGANO) NA WASANII 50 WATANZANIA WAMEHUSIKA KWENYE NYIMBO HIYO

Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa na wasanii 50, kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki kama Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja, na kwa ushirikiano mkubwa, wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu. Baadhi ya Wasanii waliohusika ni Amini, Kadjanito, Mwasiti, Linah, Christina Shusho, Khadija Kopa, Frola Mbasha, Ommy Dimpoz, Diamond, Josse Mara, Kalala Jr,
Ali Kiba, Peter Msechu, Mrisho Mpoto na Abdul Kiba. Wengine ni Mzee Yusuph, Angel, Mwana Fa, Nikki Wa pili, G Nako, Godzilla, Madee
Asley, Shaa, Mandojo, Domokaya na Shilole.

No comments

Powered by Blogger.