KALI YA MWAKA: MAKAMU WAZIRI MKUU WA UTURUKI APIGA MARUFUKU WANAWAKE KUCHEKA HADHARANI


Wanawake nchini Uturuki wanapost picha zao kwenye mitandao ya kijamii zinazowaonesha wakicheka. Kwanini?

Kwa mujibu wa makamu waziri mkuu wa Uturuki Bulent Arinc, wanawake hawatakiwi kucheka hadharani. Maoni yake aliyoyatoa Jumatatu hii yamesababisha upingwaji mkubwa ambapo wanawake nchini humo wametumia Twitter na Instagram kupost picha wakicheka kumdhihaki.

Hadi sasa kuna zaidi ya 300,000 zinazotumia neno “kahkaha” – lenye maana a kicheko na hashtag kama “Resist Laughter” (#direnkahkaha) na “Resist Woman” (#direnkadin). Wengi wanadai kuwa serikali inapaswa kushughulika na masuala muhimu kama ubakaji, ukatili wa nyumbani, na ndoa za wasichana wenye umri mdogo na sio kuzuia wanawake kucheka hadharani.

No comments

Powered by Blogger.