PICHA: MASHABIKI WA MPIRA WANAOIUNGA MKONO PALESTINA WAVAMIA WACHEZAJI WA MACCABI HAIFA YA ISRAEL UWANJANI

 MECHI kati ya timu Israeli ya Maccabi dhidi ya Lille ya Ufaransa iliahirishwa baada ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina kuvamiwa uwanja.
Waandamanaji hao walioripotiwa kuwa na asili ya Uturuki waliingia katika uwanja wa Austrian ambapo mchezo ulikuwa unaendelea na kuwavamia wachezaji wa Maccabi na kuzua vurugu.
Mmoja wa wachezaji alionekana akizozana na shabiki kabla ya kuanza kurushiana makonde mazito. Hata hivyo wachezaji wa Maccabi walifanikiwa kutoka uwanjani bila kujeruhiwa. Tukio hili limekuja wakati huu ambao majeshi ya Israel yamevamia na kufanya uhalifu dhidi ya majeshi ya Hamas huko Gaza.

No comments

Powered by Blogger.