WANAJESHI WAKABIDHI VIFAA VYA KUTUNZIA KUMBUKUMBU(BLACK BOX) VYA NDEGE ILIYOLIPULIWA NCHINI UKRAINE

Mwanajeshi wa wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi akikabidhi mojawapo ya vifaa vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia MH17 iliyolipuliwa kwa maofisa wa Malaysia.
HATIMAYE wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi wamekabidhi vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege MH17 ya Malaysia iliyolipuliwa kwa maofisa uchunguzi wa Malaysia huko Ukraine.
Vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia vilivyokabidhiwa.

ENDELEA KUSOMA HABA HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI

 
Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni baada ya wito mbalimbali kutolewa kuhusu maofisa wa uchunguzi kuruhusiwa kufanya uchunguzi wao eneo hilo la ajali iliyouwa watu 298. Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ameeleza kuwa vifaa hivyo vilikabidhiwa mjini Donetsk jana baada ya mazungumzo ya muda mrefu na wapiganaji hao.
Mtaalamu wa Malaysia akikagua moja ya vifaa hivyo.
Vifaa hivyo vikiwekwa kwenye mfuko baada ya makabidhiano.

No comments

Powered by Blogger.