WAUMINI WA ORTHODOX NCHINI UKRAINE SASA KUSALI/KUINGIA KANISANI KWA KUTUMIA APP YA IPHON

Kanisa la Orthodox nchini Ukraine limeanza kutumia smartphones kuwawezesha waumini kusali/kuingia kanisani wakiwa majumbani mwao.

Kanisa la Svyato-Troyitskyy (Utatu Mtakatifu) kwenye wilaya ya Troyeshchyna iliyopo Kieve nchini humo, limeikubali app ya iPhone iliyotengenezwa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha historia cha Kiev Volodymyr Shemarov.
Kijana huyo mwenye miaka 21 anadai kuwa app hiyo ni ya kwanza katika kanisa lolote lililopo nchini humo.
“Vijana huenda mara chache sana kanisani, wanapenda kukaa kwenye computer zao na kutembelea mitandao ya kijamii,” anasema kijana huyo. “Nataka kutumia mapenzi yao kwa kuwapa kanisa kwa kutumia teknolojia ya simu.”
App hiyo inakuwezesha kuingia kwenye kanisa la mtandaoni na kusali na kuomba ushauri kwa padre na pia kuangalia muda wa misa. Mapadre wao wenyewe wanaipromote sana app hiyo kwa kuitangaza kanisani wakati wa misa.

No comments

Powered by Blogger.