CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHAKANUSHA TAARIFA YA DIAMOND KUTUNIKIWA PHD

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Diamond akiwa kwenye moja ya show zake
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala amekanusha taarifa zilizozagaa zinazodai kuwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz atatunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) kutokana na mchango wake kwa jamii.
Akizungumza na Power Jams ya East Africa Radio, Prof. Rwekaza Mukandala ambae yupo nje ya nchi kwa sasa amesema taarifa hizo si za kweli ni uzushi tu.
“Hizi tetesi ni za uvumi, si za kweli,” alinukuliwa na mtangazaji wa radio hiyo ambapo alidai walishindwa kuelewana vizuri kutokana na mawasiliano kuwa si mazuri.
Hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliibuka taarifa iliyosema: Katika mahafali ya 44 ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yatakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City tarehe 08 November 2014, aliyekuwa mkuu wa chuo (Chancellor) wa UDSM marehemu Balozi Fulgence Kazaura na msanii maarufu Afrika aliyeshinda tunzo nyingi zaidi kuliko wasanii wote Tanzania Diamond Platinumz watatunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (Honoris Causa) ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mchango wao kwenye jamii.

No comments

Powered by Blogger.