TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. 


Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48  kwa siku za Alhamisi na Ijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo. 

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; 
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. 

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.       
Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.
Au piga simu huduma kwa wateja namba 022- 2194800  / 0658-198889
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na ofisi ya uhusiano, 
Dawasco - Makao Makuu.

No comments

Powered by Blogger.