VIDEO NA PICHA: AZIKWA AKIWA AMEKAA KWENYE JENEZA NCHINI KENYA

Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.

Habari kutoka Kenya inahusiana na mazishi ya aina yake ambapo familia moja imefanya mazishi ya mzee wao aliyekuwa akifahamika kwa jina la Adriano Aluchio anayetajwa kuwa mzee wa kuheshimika kwenye jamii hiyo akiwa amekaa ndani ya jeneza lilichongwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.
Baadhi ya watu waliohojiwa kuhusiana na tukio hilo wamesema ni utamaduni wa jamii ya kabila la Lughia kufanya mazishi ya namna hiyo kwa mzee aliyeheshimika, kwa imani kuwa amefariki lakini anaendelea kuwalinda watoto wake pamoja na jamii yake.

ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
Moja ya wazee katika jamii hiyo amenukuliwa akisema, “Mazishi kama hayo ya kumkalisha marehemu yalianza tangu zamani sana wakati wa mfalme Nabongo Mumia, na sisi tulitokea katika jamii hiyo, tukimzika amelala hatoridhika… Ataonekana akitembea huku juu….”
Baada ya mazishi hayo ya kipekee, walichukuliwa ng’ombe dume wawili na kupiganishwa juu ya kaburi kama njia ya kufukuza mapepo wachafu, huku wanakijiji wakipongeza kitendo cha mzee huyo kupewa mazishi ya hadhi.
Jamii ya Waidakho katika kabila la Walughia wanoishi katika kaonti ya kakamega wanajulikana sana kwa mchezo wao unaowavutia watalii eneo hilo la kuwapiganisha Fahali na kuku Jogoo.

No comments

Powered by Blogger.