UKAWA WATANGAZA RASMI KUSUSIA VIKAO VYOTE VYA BUNGE VILIVYOBAKI KUTOKANA NA UKIUKWAJI WA KANUNI
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255713363965 / +255755274953. Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Umoja wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) leo umetangaza rasmi kususia
vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo
huo mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi wa kambi rasmi
ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema wabunge wote kutoka katika vyama
vinavyounda umoja huo hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao kuwa
hawajaadhibiwa.
Umoja huo pia
umemtaka Rais Kikwete kutotia saini muswada hiyo kwa kuwa imepitishwa kinyume
cha taratibu. Mbowe amesema kuwa
endapo Rais Kikwete atalazimisha kuisaini miswada hiyo, umoja huo utaishitaki
serikali kwa wananchi.
Wabunge wote kutoka
UKAWA wameazimia kuondoka kabisa leo kutoka mjini Dodoma, na wanataraji
kukutana jijini Dar es salaam siku ya Jumatano kwa hatua zaidi.
Wakati huo huo
bunge limepitisha muswada wa usimamizi wa mapato yatokanayo na mafuta na gesi,
na muswada mwingine wa uwazi na uwajibikaji katika uchimbaji wa madini, gesi na
mafuta, hiyo ikiwa ni miswada miwli kati ya mitatu ambayo imekuwa ikipingwa na
wabunge kutoka UKAWA.
Muswada mwingine ni
ule wa sheria ya Petroli ambao ulipitishwa jana bila ya ushiriki wa wabunge hao.
CHANZO: JAMII FORUM
Post a Comment