ABIRIA WANUSURIKA KIFO KWENYE BASI LA SAI BABA BAADA YA KUPASUKA TAIRI
Basi liliweza kusimama salama na hakuna mtu yeyoye aliyejeruiwa katika ajari hiyo( Picha na Michuzi Blog)
ABIRIA wapatao 45 waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Sai baba,kutoka Jijini Dar es salaam kwenda Masasi,mkoani Mtwara,wamenusulika kifo,kufuatia gari yao kuacha njia na kutumbukia mtoni.
Tukio la ajali hiyo limetokea maeneo ya kijiji na kata ya Mbanja,iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Katika
ajali hiyo watu watano akiwemo dereva na kondakta ndiyo waliokuwa
wameumia na kukimbizwa Hospitali ya mkoa ya Sokoine kwa matibabu.
Waliojeruhiwa
ni,Juma Mtoi (Dereva),Said Mkumbwa (Kondakta) wakazi wa Jijini Dar es
salaam,na kwa upande wa abiria ni John Kasawala (21),mkazi wa kijiji cha
Nangamba,wilaya ya Nanyumbu,mkoani Mtwara,Noel Akui (35) mkaazi wa
wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara na Kuruthumu Ally (25) wakazi wa mji wa
Lindi.
Said
Mkumbwa ambaye ni kondakta wa basi hilo, amesema kwamba chanzo cha
ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la mbele upande wa kulia kwa dreva,
ambapo liliacha njia na kutumbukia mtoni chini ya daraja la
Mbanja. Akasema
basi lake lililokuwa limebeba abiria 45 lilikuwa likitoka Jijini Dar es
salaam kuelekea wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,kufuatana na ruti zake.
“Tulikuwa
tikitokea Dar es salaam kwenda Masasi,kwani ndiyo ruti yetu ilivyo, na
ndipo tulipofika eneo hilo mpira wa tairi ya mbele upande wa dereva
likapasuka na kukosa mwelekeo kisha likagonga kingo ndogo ya
daraja na kutumbukia mtoni,,,,,,,,,tunachoshukuru ni kwamba wote tumetoka tukiwa hao hakuna aliyepoteza maisha”Alisema Mkumbwa.
Kuruthumu
Ally ambaye amepata michubuko kiasi usoni na mabegani na John Kasawala
aliyeumia kichwani,kwa nyakati tafauti walisema wao walikuwa wamekaa
sehemu ya mbele na ghafla walisikia mlio mkubwa kisha basi lao kuyumba
na kutumbukia chini ya daraja.
Akizungumza
kwa niaba ya kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dkt,Edgar Mlawa
amesema majeruhi hao wameumia sehemu mbalimbali ya miili yao,ikiwemo
vichwani na hali zao zinaendelea vizuri na kuna mategemeo ya kuweza
kuendelea na safari zao kama kawaida.
“Hapa
Hospitalini wamefikishwa majeruhi watano tu,akiwemo dereva,kondakta
wake na abiria watatu,mmoja wao ni mwanamke, ambapo wote hao hakuna
aliyekuwa sirias kwa kuumia licha ya kupata majeraha sehemu mbalimbali
ya miili yao.ikiwa ni pamoja na vichwani”Alisema Dkt,Mlawa.
Post a Comment