WAKAZI WA MTAA WA NJEDENGWA KUANDAMANA KUELEKEA BUNGENI

 Mwananchi aliyekuwa na silaha kwenye tukio la bomoabomoa.lililofanyika Njedengwa Dodoma Oktoba 2011. 5
 
  Hayo yalisemwa na mmoja wa wananchi hao Bi. Rehema Mgwanyi mbele ya Diwani wa kata ya Dodoma Makulu Chief Ally Bilingi nje ya kanisa la Anglican, walipokuwa wamekusanyika kusubili mkutano waliokuwa wametangaziwa kuwa utafanyikia eneo hilo ambao hata hivyo uliota mbawa kutokana na kutofika kwa viongozi husika bila taarifa yoyote. Mgwanyi alisema walikusanyika eneo hilo kuanzia saa mbili asubuhi ili kuhudhuria mkutano huo ulioitishwa na viongozi wao lakini cha kushangaza mpaka muda huo wa saa sita hakukuwa na kiongozi yoyote alikuwa amefika ndipo wakaamua kumpigia Diwani  na alipofika wakamwambia wao wamechoka kupigwa Danadana hivyo ni Bora waandamane kwenda Bungeni. 

‘’Diwani sisi tumechoka Bunge  linaloanza keshokutwa tunaandamana kuelekea pale tukawaone viongozi wakuu wa serekali tuwaambie kuhusu ubadhilifu wa viwanja 99,  bomba la maji, na kutoitwa mikutano kama je ni halali kisheria kutoitishwa mikutano kwa miaka hiyo 3’’, alisema
Diwani Chief Ally Bilingi alisema  kama wananchi wameamua kuandamana ili kwenda kutafuta haki yao wanapofikili watapaipata hataweza kuwazuia bali atawaelekeza wafuate utaratibu kama kweli watafanyahivyo maana hata yeye hakuwa anajua kama kuna mkutano ama umeahirishwa.

‘’ni kweli huu ni ubabaishaji kwa wanchi maana mimi mwenyewe nilipata taarifa nilipokuwa kwenye mambo yangu ya kawaida manispaa, Mkurugenzi Robert Kitimbo aliniambia alikuwa aje kusimamia mkutano leo lakini alipata dharula ya safari ya kikazi Dar lakini aliahidi mwishoni mwa wiki la kwanza la Bunge utafanyika’’, alisema
Aidha Bilingi aliwataka  viongozi wa kata hiyo kutokuwa na usiri wa kutomshirikisha mambo ya msingi kuhusu kata anayoiongoza kwani yeye ni rahisi kuwasiriana na wanachi wa kata hiyo kuliko mtu yoyote, watendaji  na Mwenyekiti waliletwa ili wasaidie kuleta maendeleo kwa niaba ya Serekali hivyo wasikilize na kutoa majibu ya wananchi bila Brabra.

Kwa upande wake Mtendaji wa kata hiyo ya Dodoma Makulu Magreth Songolo ambaye amekuwa akionyesha kutojua wajibu wake wa kiutendaji alipoulizwa kama mkutano uliahilishwa mpaka lini na kwanini hawakuwajulisha wanchi  alisema yeye hana majibu Bali mkurugenzi wa manispaa Robert Kitimbo, alipoambiwa Kitimbo amesema Mtendaji anaweza kutoa ufafanuzi akasema afuatwe ofisini kwake na wananchi wafanye chochote yeye haimhusu.

HABARI NI KWA HISANI YA  JOHN BANDA, DODOMA

No comments

Powered by Blogger.